Slider

TPA YATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA KISARAWE
Local News

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa Vitanda 20, Magodoro 20 na Shuka 100 kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.   Vitanda hivyo vya kisasa aina ya ‘Cardiac, mashuka pamoja na magodoro yake vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo ya wilaya vina thamani ya shilingi za kitanzania milioni 13.   Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi amesema msaada huo ni sehemu ya wajibu wa Mamlaka kuisaidia jamii ya Watanzania.  ...

Like
366
0
Monday, 21 March 2016
ZOEZI LA KUHESABU KURA LAENDELEA ZANZIBAR
Local News

ZOEZI la kuhesabu kura linaendelea visiwani Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana. Imeelezwa kwamba idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza kushiriki katika uchaguzi huo ambao ulisusiwa na baadhi ya vyama vikuu vya upinzani. Nchi nyingine za Afrika ambazo zimefanya Uchaguzi jana ni pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Niger na nchi ya Cape Verde ambapo tayari chama kikuu cha upinzani nchini humo MPD kimeshinda baada ya uchaguzi wa jana kwa zaidi ya asilimia 53 huku mkuu wa...

Like
287
0
Monday, 21 March 2016
HATIMAYE ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA HADHARANI
Slider

Kwa mara ya kwanza Manchester City yafuzu katika hatua hiyo ikikutana na vigogo kutoka nchini Ufaransa Paris St-Germain, Vita nyingine kali ni kati ya mabingwa wa Hispania Fc Barcelona dhidi ya majirani zao Atletico Madrid, huku Bayern Munich na Real Madrid wakipata mchekea. Wolfsburg (Germany) v Real Madrid (Spain) Bayern Munich (Germany) v Benfica (Portugal) Barcelona (Spain) v Atletico Madrid (Spain) Paris St-Germain (France) v Manchester City (England) Michezo hiyo inapigwa Tarehe 5 – 6 April na Marudiano ni Tarehe...

Like
347
0
Friday, 18 March 2016
BRAZIL: MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUTAWANYA WAANDAMANAJI
Local News

POLISI nchini Brazil wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwazuia waandamanaji kutoka makao makuu ya rais Dilma Roussef. Maelfu ya watu wanaotaka aachie madaraka waliandamana katika mji mkuu Brasilia. Wanamlaumu rais Roussef na chama chake cha workers party kwa ufisadi, lakini pia kulikuwa na maandamano ya kumpinga Roussef katika mji mkubwa zaidi nchini Brazil wa Sao...

Like
274
0
Friday, 18 March 2016
KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MAWILI YA MASAFA MAREFU
Global News

TAIFA la Korea Kaskazini limerusha makombora mawili ya masafa marefu katika bahari ya mashariki ya pwani yake, siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong-un kuagiza majaribio ya mabomu zaidi ya kinyuklia na silaha nyingine. Marekani imejibu kwa kutoa wito kwa Pyongyang kutozua wasiwasi katika eneo hilo ambao umekua juu tangu Korea Kaskazini ifanye jaribio la nne la mabomu yake ya kinyuklia mnamo mwezi Januari. Korea Kusini imeelezea jaribio hilo la hivi karibuni kama tishio kubwa la usalama na udhibiti...

Like
397
0
Friday, 18 March 2016
TASAF YAPATIWA DOLA MILIONI 665 KUNUSURU KAYA MASIKINI
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.   Mkataba huo ambao umetiwa saini jijini Dar es Salaam unawataka watendaji kuweka utaratibu ambao unaenda sambamba na Mpango wa utekelezaji bila kuingilia majukumu ya mamlaka ya Serikali katika utekelezaji wa TASAF wa kunusuru kaya masikini.   Akizungumzia mkataba huo mara baada ya kusaini kwa niaba...

Like
264
0
Friday, 18 March 2016
RAIS MAGUFULI AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa Hospitali ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi-CCM-kwa wananchi wa Jimbo hilo. Akikabidhi gari hilo leo Ikulu Jijini Dar es salaam kwa mbunge wa Jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Rais ikiwa ni kuitikia wito wa...

Like
354
0
Friday, 18 March 2016
JWTZ YAKANUSHA KUPELEKA MAJESHI ZANZIBAR
Local News

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi wa marudio unaotarajia kufanyika Machi 20 mwaka huu.   Jeshi hilo limesema kuwa Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma kwani JWTZ lina Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa Taifa hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale...

Like
329
0
Thursday, 17 March 2016
WZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 2 CHATO
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.   Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, bwana Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Dioniz Mutayoba.   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana usiku alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano...

Like
433
0
Thursday, 17 March 2016
TRUMP APETA MAJIMBO MUHIMU MAREKANI
Global News

DONALD TRUMP amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo katika majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida.   Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.Hata hivyo ameshindwa na John Kasich katika jimbo la Ohio.   Mgombea anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North...

Like
316
0
Wednesday, 16 March 2016
MCHAKATO WA KUMALIZA KERO YA MIUNDOMBINU WAANZA KUFANYIWA KAZI TANDIKA
Local News

DIWANI wa kata ya Tandika Ramadhani Litumangiza amesema kuwa mchakato wa kuimaliza kero kubwa ya miundombinu ya barabara za ndani ya mtaa huo ambazo zimekuwa na mashimo na kutopitika kipindi cha mvua umekamilika na kuanza kufanyiwa kazi hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Tandika jijini Dar es salaam, Diwani Ramadhani amesema kuwa kumekuwa na kero hiyo ambapo kipindi cha mvua maji hujaa kwenye madimbwi yaliyopo barabarani na kuingia kwenye nyumba za watu. Ameongeza kuwa tayari amefanikiwa kupata...

Like
363
0
Wednesday, 16 March 2016