MGOMBEA Urais Donald Trump ameshambuliwa na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono. Bwana Trump anayeongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz. Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si...
UTABIRI wa Hali ya Hewa kwa mvua za masika zinazoanza wiki hii nchini umeonesha kuwa zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi huku baadhi ya maeneo zikiwa chini ya wastani. Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi mkuu wa malaka ya Hali ya Hewa Tanzania dokta Agnes Kijazi ambapo amesema katika maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria, Nyanda za juu, Kaskazini Mashariki pamoja na maeneo machache ya mkoa wa Tanga mvua zitanyesha hadi juu...
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Waziri mkuu Majaliwa mefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa...
KOREA KASKAZINI imerusha makombora ya masafa mafupi, baharini kujibu vikwazo vipya ilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jeshi la Korea Kusini limethibitisha kushuhudia shughuli hiyo na kusema kwamba havikulenga mtu yeyote. Miongoni mwa vikwazo vipya vilivyowekwa na umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo ni pamoja na kuhakikisha mizigo yote inayoingia Korea Kaskazini kutoka nje kuanza...
IKIWA tayari mwelekeo unaonesha kuwa kinyang’anyiro cha kiti cha urais wa Marekni kitakuwa ni kati ya Bi. Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican, wazee na vigogo ndani ya chama cha Republican wamesema kuwa hawapo tayari kumruhusu Trump Agombee Urais. Wakuu hao wa chama cha Republican wamesema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais wao basi kuna uwezekano mkubwa wa chama chao kusambaratika. Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South...
WAZAZI na Walezi nchini wametakiwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na ndugu au wanafamilia dhidi ya watoto wa kike na hata wa kiume ili wachukuliwe hatua. Akizungumza na Efm Mwanasheria Msaidizi wa Jaji kutoka Chama cha Majaji Wanawake Tanzania-TAWJA-Koku Mwanemile ameeleza kuwa kufumbia macho vitendo hivyo kunachangia kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji kwa watoto. Koku amebainisha kuwa endapo wazazi, walezi na jamii wataungana pamoja kwa kufichua vitendo hivyo vinavyosababisha athari kubwa kwa...
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao za kuisaidia serikali. Makamba ametoa wito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam. Makamba amesema kamati hiyo ni muhimu katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe...
UMOJA wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji unaoendelea kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia, ambako polisi wa Macedonia waliwafyatulia mabomu ya kutoa machozi mamia ya wahamiaji. Msemaji wa halmashauri kuu wa umoja huo Margaritis Schinas, amesema matukio yalioonyeshwa kwenye mpaka huo siyo njia sahihi ya kushughulikia mgogoro huo. Naye Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema matukio hayo yanaonyesha umuhimu wa mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya umoja wa Ulaya wa kujadili mgogoro wa...
IMEELEZWA kuwa aliyekuwa kiongozi wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa dola milioni 29 za kulifadhili kundi la Jihad kabla ya kuuawa mwaka 2011. Kwa mujibu wa wosia wake aliouandika ambao umeonekana leo ameihimiza familia yake kuheshimu wosia wake na kuwashauri watumie mali yake yote kuendeleza kundi la jihad. Mali yake na wasia wake ni miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa leo na maafisa usalama wa Marekani ambao pia wosia huo...
BENKI ya Bacley’s Tanzania imekanusha taarifa ambazo sio sahihi juu ya kusitishwa kwa huduma zake kwa madai kuwa Benki hiyo imeuzwa kwa nchi za Afrika. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijni Dar s salaam jana wakati wa kutoa ripoti ya Benki hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, mkuu wa idara ya masoko wa Bacley’s JOE BENDERA amesema kuwa Benki hiyo inaendelea kutoa huduma kwa wateja wake kwa ufasaha na inaendelea kuboresha zaidi....
JAMII nchini imeombwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kupunguza vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto hao. Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Afisa Ustawi wa jamii Neema Mambosho wakati alipokuwa akizungumza na E FM juu ya ongezeko la watoto wa mtaani. Amesema kuwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za ukatili na kunyanyapaliwa hivyo jamii inapaswa kuelimishwa ili kuzuia vitendo...