KUNDI la kislamu la Islamic State limesema kuwa limetekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Syria Damascus na mji wa Homs, na kusababisha vifo vya watu 140. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya Habari zimeeleza kwamba Mapema huko Homs watu 57, wengi wao raia wa kawaida wameuawa katika mashambulizi mawili ya magari. Mashambulizi hayo mawili yamelenga maeneo yaliyozingirwa na waislamu wachache, kama ilivyoelezwa na kundi la waislamu la Sunni la...
KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi nchini humo. Watu walioshuhudia kukamatwa kwake wamesema kwamba Kizza amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake alipokuwa amewekwa kizuizini. Awali kulikuwa na habari kwamba kiongozi huyo angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuonesha matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais ingawa tayari Tume ya Uchaguzi ilishamtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki...
WAKATI Serikali kupitia Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ikiendelea na mpango wa kufukuza wafanyakazi wasiokidhi viwango vya utendaji kazi kwa kutumia Kauli ya Kutumbua Majipu iliyoanzishwa na Rais wa Awamu ya Tano Dokta John Pombe Magofuli, Wananchi wengi wameonesha kuunga mkono hatua hiyo. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa mazoea na kufanya Ofisi na Taasisi za Serikali kama mali zao hivyo kitendo cha kuwaondosha kitasaidia kuongeza...
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora mheshimiwa Angela Kairuki amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi waliopo chini yake. Kairuki ametoa maagizo hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa Habari katika mkutano ulifanyika chuoni hapo. Aidha amebainisha kuwa usimamizi mbovu wa bwana Nassoro umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za...
TAKRIBAN watu 140 wameuawa kwa milipuko ya mabomu katika miji ya Homs na Damascus nchini Syria, waangalizi na vyombo vya habari vya serikali wameeleza. Inaelezwa kuwa milipuko minne ilitokea katika eneo la Sayyida Zeinab mjini Damascus na kuua takriban watu 83, ambapo awali mjini Homs Watu 57 wengi wao raia waliuawa kwa mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye magari mawili. Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kutekeleza mashambulizi hayo katika miji hiyo yote...
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema uchaguzi uliofanyika nchini humo Alhamisi wiki iliyopita ulikuwa wa haki na akasema wanaoutilia shaka hawaielewi Uganda. Aidha, ametetea hatua ya maafisa wa usalama kumzuilia mgombea mkuu wa upinzani Dkt Kizza Besigye wa chama cha FDC. Tume ya Uchaguzi ilisema Jumapili kwamba Bwana Museveni alipata ushindi wa asilimia 60.75 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Dkt Besigye aliyepata asilimia 37.35, lakini upinzani umedai kuwepo wizi wa kura na waangalizi wa kimataifa wamesema pia kwamba...
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari. Kwa mujibu wa TAMWA, utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo. Takwimu hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea na...
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, leo anatarajia kuzitembelea kaya zaidi ya 145 zilizoathiriwa na mafuriko katika kata ya Pawaga, wilayani Iringa kwa lengo la kuzifariji. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu anatarajiwa kuambatana na Mbunge wa Jimbo la Isimani ilipo kata hiyo, William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambao kwa pamoja watajionea hali halisi ya maisha ya kaya hizo zinazoendelea kusaidiwa ili zirudi katika maisha yake ya kawaida. Hata hivo mkuu wa wilaya ya Iringa,...
MATOKEO ya awali yaliyotangazwa hii leo nchini Uganda yanaonyesha rais wa muda mrefu wa nchi hiyo amempita mpizani wake mkuu katika uchaguzi wa rais nchini humo. Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya Uganda, rais Yoweri Kaguta Museveni amejipatia takriban asilimia 62 ya kura, akimpita mpinzani wake mkubwa Kizza Besigye aliyejipatia asili mia 33 ya kura. Matokeo hayo yanahusu asili mia 23 ya vituo vyote vya kupiga kura nchini humo ambapo Matokeo ya...
BAADA ya Baraza la mitiani Tanzania NECTA kutangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 ,Wanafunzi wa shule ya sekondari pamba jijini Mwanza wameeleza kufurahishwa kwa mfumo wa ufaulu wa divisheni tofauti na mfumo uliokuwepo wa GPA . Wakizungumza na Efm baadhi ya wananfunzi hao wamesema kuwa matokeo hayo yanaonyesha namna mfumo wa divisheni unavyo pima uwezo wa wanafunzi darasani. Wakizungumzia mfumo wa GPA wamesema mfumo huo ulikuwa unawafanya wanafunzi kuzembea katika masomo yao wakiamini kuwa watafaulu hali ambayo imekuwa kinyume na...
SERIKALI imeombwa kuisaidia jamii ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kuhakikisha wanapata elimu kwani hadi sasa ni asilimia 10 pekee ndiyo wanaopata elimu. Akizungumza na kituo hiki Katibu wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) amesema kuwa Tanzania ina zaidi ya watu million sita wenye ulemavu mbalimbali hivyo ni vema wakasaidiwa kupata elimu ili kuondokana na tatizo la kuitegemea jamii na serikali kuwasaidia kuyaendesha maisha...