Efm Radio,katika harakati zakufanikisha ahadi ya kujenga madarasa, imekabidhiwa michoro ya ramani ya madarasa ya sekondari wilaya ya Kinondoni kata ya Kimara, Makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Kituo hicho cha Utangazaji kupitia masafa ya 93.7 leo asubuhi. Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio, Francis Siza akipokea ramani ya michoro ya madarasa kutoka kwa Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bwana Rogers J. Shemwelekwa. Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Rogers J. Shemwelekwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Efm...
WATU zaidi ya 70 wameuawa kutokana na mashambulio ya mabomu ambayo kundi la magaidi wanaoitwa Dola la Kiislamu limedai kuyafanya karibu na sehemu takatifu ya Washia nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kituo kilichopo mjini London, kinachofuatilia haki za binadamu nchini Syria, watu hao waliuawa kutokana na miripuko miwili ya mabomu karibu na sehemu hiyo takatifu, Sayyida Zeinab. Watoto kadhaa walikuwamo miongoni mwa walioangamizwa huku Watu wengine zaidi ya 100...
NIGERIA imeomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu na nusu kutoka Benki ya Dunia ili kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake. Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani. Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani...
RAIS wa Jamhuri ya Mmuungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili. Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa tukio hilo ambapo...
SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeona picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi. Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura. Shirika hilo limeongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku...
KUNDI la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi kwa mahakama ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba. Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo. Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama...
SHIRILA la maendeleo ya mafuta na petrol Tanzania (TPDC) kwa kushrikiana na kampuni tatu wanatarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea katika wilaya ya kilwa mkoani lindi. Akizungunza wakati wa semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uelewa wa sekta ndogo ya mafuta na gesi mkurugenzi wa mkondo wa chini kutoka TPDC dokta Wellington Hudson amezitaja baadhi ya kampuni watakazoshirikiana nazo katika ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni pamoja na kampuni ya ferostar ya Ujerumani na haldo...
SERIKALI imewahakikishia wananchi hususani wavuvi wadogo kuwa itahakikisha inawawezesha wavuvi hao kufanya shughuli zao za uvuvi kwa manufaa ili kujiletea maendeleo yao pamoja na Taifa kwa ujumla. Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Mwibara mheshimiwa Kangi Lugola aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kuwanufaisha wavuvi. Katika majibu ya swali hilo pia mheshimiwa Nchemba amewataka watu wenye dhamana ya kusimamia shughuli...
MAHAKAMA Kuu mjini Mombasa imeamua kwamba washukiwa wawili walioshitakiwa kwa mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni miaka miwili iliyopita wana kesi ya kujibu. Jaji Martin Muya amesema upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka wawili hao. Diana Salim Suleiman na Mahadi Suleiman Mahadi ajulikanaye kama Jesus wanadaiwa kuhusika katika uvamizi uliopelekea kuuawa kwa watu 60 mwezi Juni mwaka 2014 katika vijiji vya Mpeketoni na Kaisairi, Kaunti ya Lamu.nchini Kenya....
WAZIRI wa uchumi nchini Japan Akira Amari amejiuzulu kutokana na madai ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili. Bwana Amari ametoa tangazo hilo ghafla katika mkutano na waandishi wa habari jana ambapo mbali na hayo amekanusha kupokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi kama ilivyodaiwa na jarida moja la Japan. Hatua hiyo imechukuliwa kama pigo kubwa kwa waziri mkuu Shinzo Abe kwani Amari alitarajiwa kusafiri hadi New Zealand wiki ijayo kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa ya ng’ambo ya pili ya...