KANALI WA JESHI AUAWA BURUNDI
Global News

KANALI mmoja wa Jeshi amepigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura,kulingana na vyombo vya habari vya kundi la SOS nchini humo. Kanali Emmanuel Buzubona aliuawa pamoja na mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki siku ya Jumatano kaskazini mwa makaazi ya mji huo. Ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wa hivi karibuni kuuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kunusurika jaribio la mapinduzi na maandamano kufuatia hatua yake ya mwaka jana kujiongezea muda wa kuhudumu kama rais wa taifa...

Like
224
0
Thursday, 21 April 2016
UCHAGUZI MKUU 2015: WADAU WAIPONGEZA NEC
Local News

WADAU mbalimbali kutoka vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendesha zoezi hilo kwa Uwazi, Haki, Amani na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni. Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha NRA Hassan Kasabya alipokuwa akitoa pongezi kwa Tume hiyo kwa kutoa vyeti vya shukrani kwa washiriki hao kutoka vyama vya siasa na wadau...

Like
209
0
Thursday, 21 April 2016
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AAPISHWA RASMI LEO
Local News

MKUU wa mkoa wa Dar es salaamu mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amemuapisha rasmi mteule mkuu wa wilaya ya kinondoni ALY SALUM HAPI ambapo amemtaka kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele kutimiza matakwa ya mheshimiwa rais ikiwemo kupinga ufisadi na rushwa . Awali akizungumza mbele ya watendaji ,wakuu wa wilaya na wakuu wa ulinzi na usalama, mheshimiwa PAUL MAKONDA amesema licha ya kuwa na umri mdogo inatakiwa atumie nafasi alio aminiwa na mheshimiwa rais kutekeleza majukumu hasa kuhakikisha kunakuwepo na haki kwa...

Like
289
0
Thursday, 21 April 2016
YANGA, TP MAZEMBE NJE MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA
Slider

Wakicheza Ugenini huko Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Al Ahly na kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa Africa. Mabingwa watetezi Tp Mazembe wakaondolewa katika michuano hiyo baada ya sare ya 1-1 dhidi Wydad de Casablanca, na Casablanca wakisonga mbele kwa ushindi 3-1. Enyimba wakasonga mbele kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Etoile du Sahel ,As Vita Club nao wakasonga mbele licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 na Mamelod Sundowns . Al Ahli Tripoli wakawachapa Asec Mimosas kwa mabao...

Like
298
0
Thursday, 21 April 2016
WAKIMBIZI 500 WAHOFIWA KUFA KWENYE BAHARI YA MEDITERANIA
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia wakimbizi limehofu kuwa huenda wakimbizi 500 wamefariki kwenye bahari ya Mediterania walipokuwa njiani kuelekea Italia. Hata hivyo msemaji wa shirika hilo amewaambia waandishi wa habari kwamba haijulikani ni lini wakimbizi hao wamefariki lakini amesema wachunguzi wanawahoji wakimbizi 41 walionusurika. Umoja wa Mataifa umebaisha kwamba miongoni mwa watu waliookolewa walikuwa wakimbizi kutoka Somalia, Ethiopia, Misri na...

Like
299
0
Thursday, 21 April 2016
2 WACHOMWA MOTO ZAMBIA KWENYE VURUGU
Local News

POLISI nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni. Watu Zaidi ya 250 wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyarwanda kuvamiwa. Uvamizi huo umetokea baada ya wanyarwanda hao kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja....

Like
284
0
Thursday, 21 April 2016
MHANDISI MANISPAA YA ILALA NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA
Local News

MANISPAA ya Ilala Jijini Dar es salaam imemvua madaraka mkuu wa Idara ya ujenzi mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kujengwa chini ya kiwango.   Akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amewataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajali Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi.   Kuyeko amesema baraza la madiwani...

Like
225
0
Thursday, 21 April 2016
MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI WA PUA, MASIKIO LEO
Local News

MADAKTARI Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania wameendesha zoezi la upasuaji wa masikio, pua, pamoja na upasuaji wa shingo na kichwa.   Akizungumzia kuhusu zoezi hilo Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya kisasa zaidi ambapo pamoja na mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari wa Muhimbili kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji....

Like
396
0
Thursday, 21 April 2016
EPL KUTIMUA VUMBI WEEKEND HII
Slider

Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo kadhaa, Jumamosi Norwich itaikaribisha Sunderland, Everton wao watakuwa wenyeji wa Southampton, Man Utd watakuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Traford , Newcastlle itamenyana na Swansea city, West Brom watawaalika Watford na Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City. Jumapili Vinara wa ligi Leicester city watakuwa nyumbani na West Ham,Bournemouthwatawaalika Liverpool na Arsenal itamenyana na Crystal...

Like
239
0
Friday, 15 April 2016
KURA YA KUMTIMUA ROUSSEF ITAFANYIKA
Global News

MAHAKAMA ya juu zaidi nchini Brazil imekataa ombi la serikali la kutaka kutupiliwa mbali kura ya bunge kuamua ikiwa rais Dilma Rousseff ataondolewa madarakani. Mahakama imekataa kufuta amri ya kupiga kura iliyoamuliwa na spika wa bunge la chini, ambayo itaamua siku ya Jumapili ikiwa Rousseff ataondolewa madarakani au la. Wafuasi wa rais huyo, walikuwa wamedai kuwa zoezi hilo litavurugwa kwa sababu wabunge kutoka majimbo yanayompinga Rousseff huenda wakapiga kura kwanza. Bi Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa...

Like
220
0
Friday, 15 April 2016
KOREA KASKAZINI YASHINDWA KURUSHA KOMBORA
Local News

KOREA Kaskazini imefanya jaribio la kufyatua kombora katika pwani yake ya mashariki, lakini dalili zinaonesha jaribio hilo halikufanikiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani na Korea Kusini. Bado haijabainika roketi iliyotumiwa ilikuwa ya aina gani lakini inadhaniwa majaribio hayo yalikuwa ya kombora la masafa ya wastani kwa jina “Musudan” ambalo taifa hilo lilikuwa halijalifanyia majaribio. Shughuli hiyo ilikuwa ikifanyika siku ambayo ni ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa la Korea Kaskazini Kim...

Like
208
0
Friday, 15 April 2016
« Previous PageNext Page »