ASKOFU MATHIAS JOSEPH AFARIKI DUNIA
Local News

  ASKOFU msitaafu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Askofu Mathias Joseph Issuja, amefariki dunia.   Askofu isuja ambaye alizaliwa mwaka 1929 alipata daraja hilo Takatifu mwaka 1972 ambapo aliwekwa wakfu na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa na kustaafu mwaka 2005 akiwa Askofu wa Jimbo la Dodoma.   Efm imezungumza kwa njia ya simu na Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania-TEC, Padri Raymond saba ambaye amesema kuwa Askofu mstaafu Issuja, amefariki usiku wa kuamkia leo huko katika Hospitali ya...

Like
415
0
Wednesday, 13 April 2016
KESI YA HANI YAANZA AFRIKA KUSINI
Global News

KESI ya serikali ya Afrika Kusini inayopinga kuachiliwa awali kwa muuaji wa shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi Chris Hani imeanza kusikilizwa katika mahakama kuu mjini Pretoria nchini Afrika kusini. Waziri wa sheria Michael Misutha anaamini kuwa mahakama ilifanya makosa wakati ilipotoa uamuzi kuwa raia wa Poland Janusz Walus aachiliwe huru. Kuachiliwa kwake kulizua ghadhabu sehemu nyingi nchini Afrika Kusini huku Mkewe Hani akiutaja uamuzi huo kuwa ni huzuni kubwa kwa Afrika Kusini.....

Like
207
0
Tuesday, 12 April 2016
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY AWASILI LIBYA
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Italia amewasili mjini Tripoli Libya, kwa mazungumzo na kiongozi wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya Fayez Seraj. Paolo Gentiloni ni afisa mkuu wa kwanza wa bara la Ulaya kufanya ziara rasmi nchini Libya tangu utawala mpya unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kuwekwa katika mji mkuu wa Libya majuma mawili yaliyopita. Italia pamoja na mataifa kadhaa ya dola za kimagharibi yaliyoitawala Libya miaka iliyopita yameahidi kuisaidia serikali hiyo mpya kwa imani...

Like
273
0
Tuesday, 12 April 2016
JANUARY MAKAMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA BUNGE LA FINLAND
Local News

WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kamati ya fedha ya Bunge la Finland.   Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, wabunge hao wameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozifanya za kulinda na kuhifadhi mazingira.   Awali akiwakaribisha wabunge hao, Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano bora uliopo baina yake na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara yao...

Like
282
0
Tuesday, 12 April 2016
JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKISHA WANAWAKE KIKAMILIFU KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amewataka watanzania wote kutambua kwamba mafanikio na maendeleo yoyote ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla hayawezi kupatikana endapo wanawake hawataweza kushirikishwa kikamilifu kwenye vikao vya maauzi.   Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wanawake katika uongozi lililoandaliwa na taasisi ya uongozi na kuwakutanisha wanawake wa kitanzania wenye nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini....

Like
264
0
Tuesday, 12 April 2016
JESHI LAPEWA JUKUMU LA KUTENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6
Local News

JESHI La Magereza nchini na Jeshi la Kujenga Taifa wamepewa jukumu la kutengeneza madawati yenye thamani ya shilingi Bilioni 6 ambayo yatasambazwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.   Jukumu hilo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama limetolewa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi ya makabidhiziano ya mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 6 kutoka Sekretarieti ya Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania fedha ambazo zimepatikana kufuatia...

Like
240
0
Tuesday, 12 April 2016
AFISA WA KIJESHI AHAMIA KOREA KUSINI
Global News

AFISA mmoja wa kijeshi wa cheo cha juu nchini Korea Kaskazini, ambaye alikuwa akisimamia masuala ya ujasusi ameihama nchi hiyo na kuelekea Korea Kusini. Afisa huyo hajatajwa jina lakini wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini imesema kuwa alikuwa afisa wa cheo cha juu na aliondoka nchini Korea Kaskazini mwaka uliopita. Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, limenukuu taarifa zilizosema kuwa kanali huyo alitajwa kuwa shujaa sambamba na wale walioihama Korea...

Like
245
0
Monday, 11 April 2016
OBAMA AKIRI KUSHINDWA KWA SERIKALI YAKE KWENYE UTATUZI WA MZOZO WA LIBYA
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake imefeli katika kutatua mzozo wa Libya. Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake. Obama pia amesema Marekani haikuwa na mpango mahususi wa jinsi Taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar...

Like
279
0
Monday, 11 April 2016
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA TAASISI YA BASILLA MWANUKUZI BMF
Local News

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu leo amezindua rasmi taasisi ya Basilla Mwanukuzi BMF-yenye lengo la kushirikiana na Wadau ili kuwawezesha Wanawake kiuchumi. Hafla hiyo ya uzinduzi imeenda sanjari na uzinduzi wa mradi wa “Wezesha mama lishe Tanzania” ukiwa na lengo la kuwawezesha mama lishe kupata elimu ya ujasiriamali na upikaji wa chakula bora chenye kuzingatia virutubisho. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mwalimu amesema kuwa wengi waliopo katika sekta ya mama lishe ni...

Like
203
0
Monday, 11 April 2016
MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MAMA ANNA KILANGO MALECELLA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati wapo wengi.   Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.   Akizungumza baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru...

Like
296
0
Monday, 11 April 2016
MWANAHABARI WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA
Global News

MWANAHABARI aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.   Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi ya leo baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.   Hassan Hanafi, alipatikana na hatia ya kuwaua Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa shirika la habari la SONNA), Sa’id Tahlil Warsame (mkurugenzi wa HornAfrik), na Mukhtar Mohamed Hirabe (mkurugenzi wa Radio Shabelle), na wanahabari wengine...

Like
486
0
Monday, 11 April 2016
« Previous PageNext Page »