TAIFA STARS KUIVAA HARAMBEE STARS
Slider

Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi. Mchezo huo utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwezi Juni, 2016 ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Misri Juni 04, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa...

Like
227
0
Wednesday, 27 April 2016
TRUMP APETA MAJIMBO MATANO MUHIMU MAREKANI
Global News

NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican. Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani. Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode...

Like
276
0
Wednesday, 27 April 2016
WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA
Global News

SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili. Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo. Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme...

Like
232
0
Wednesday, 27 April 2016
MARA: WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KUCHANGIA MAENDELEO
Local News

WANANCHI katika halmashauri zote  mkoani mara wametakiwa kushiriki katika kuchAngia maendeleo na kuachana na dhana zinazoendelezwa na baadhi ya  viongozi katika serikali wanaotoa kauli zakuwapinga wananchi kuchangia maendeleo ya elimu na kulitumia vibaya neno Elimu bure. Yamesemwa hayo na mwenyekiti wa halmashauri ya BUTIAMA Magina Magesa alipokuwa akizungumza katika uhamasishaji wa kuchangia maendeleo ya elimu hususani ujenzi wa maaabara na madawati katika wilaya hiyo ....

Like
239
0
Wednesday, 27 April 2016
KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI KUFANYIKA IJUMAA WIKI HII
Local News

KITUO cha Uwekezaji Tanzania –TIC, kwakushirikiana na Russian Export Club kimeandaa Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.   Mbali na TIC kongamano hilo limeandaliwa pia kwa ushirikiano na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na...

Like
211
0
Wednesday, 27 April 2016
AL SHABAAB ALIYEJIUNGA NA IS ANASWA SOMALIA
Global News

KAMANDA wa kundi la al-Shabaab aliyejiunga na kundi linalojiita Islamic State nchini Somalia amekamatwa na maafisa wa usalama nchini humo.   Hassan Mohamed Siad ambaye pia hujulikana kama Hassan Fanah alikamatwa jana Jumapili baada ya maafisa wa ujasusi wa Somalia kufanya operesheni katika nyumba moja mtaa wa Kahda.   Vyombo ya habari nchini Somalia vinasema alikuwa anajificha katika mtaa huo kutoka wa wapiganaji wa al-Shabab. Serikali ya Somalia ilikuwa imeahidi zawadi ya $2,000 kwa mtu ambaye angetoa habari za kusaidia kukamatwa...

Like
200
0
Monday, 25 April 2016
ICC YAANZISHA UCHUNGUZI WA AWALI KUHUSU MAUAJI YA BURUNDI
Global News

MWENDESHA mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) amesema mahakama hiyo imeanzisha uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Burundi.   Bi Fatou Bensouda amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio ya Burundi tangu Aprili 2015 na kwamba mara kwa mara amezitaka pande zote husika kutojihusisha na ghasia na mauaji.   Watu 430 wameuawa na wengine 3,400 kukamatwa tangu kuanza kwa machafuko Aprili mwaka...

Like
211
0
Monday, 25 April 2016
MTOTO WA MWAKA MMOJA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA SHIMONI
Local News

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja aliye tambulika kwa jina la  Waziri Kashinje amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la maji wakati akicheza na wenzake katika nyumba ya jirani yao eneo la igoma Jijini Mwanza.   Akizungumza na E Fm katika eneo la tukio mjumbe wa serikali ya mtaa huo Amosi Shirangi amesema tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza na wenzake lililopo katika nyumba ya jirani.   Nao Wazazi wa mtoto huyo Kashinje...

Like
301
0
Monday, 25 April 2016
RAIS WA MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, leo amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, wawili wamebadilishiwa vituo na 13 wamebakishwa katika vituo vyao vya sasa. Makatibu tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano April 27, Ikulu saa tatu...

Like
270
0
Monday, 25 April 2016
WENGER AONYESHA HOFU EPL
Slider

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ameanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. Anasema wasiwasi zaidi unatokana na hatari ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 19. The Gunners walipoteza nafasi ya kupanda hadi nambari tatu kwenye jedwali baada ya kutoka sare tasa na Sunderland ugenini Jumapili. “Tuna haja sana na hilo na tuna wasiwasi kuhusu hilo kwa sababu sasa yatakuwa ni mapambano,” alisema...

Like
219
0
Monday, 25 April 2016
MAREKANI KUPELEKA MAJESHI SYRIA
Global News

MAAFISA wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi wa ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State. Kwa mujibu wa maafisa hao, lengo hasa ni kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria. Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano...

Like
279
0
Monday, 25 April 2016
« Previous PageNext Page »