KIGOMA: KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA RAMI MWEZI MEI MWAKANI
Local News

MAKANDARASI wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano...

Like
1150
0
Thursday, 31 March 2016
ENGLAND: ROY HODGSON AFANYA MAZUNGUMZO KUMREJESHA JOHN TERRY
Slider

Kocha wa England, Roy Hodgson akiri kuanza kufanya mazungumzo na John Terry ili arejee kwenye kikosi kuongeza nguvu. hatua ya kocha huyu kutaka kumrejesha Terry imekuja baada ya kugundua pengo kwenye safu ya ulinzi kwnye kikosi chake kwenye michuano ya Euro 2016. Terry, 35, ambae amestaafu soka la kimataifa September 2012 anatajwa kuwa tumaini la kocha Roy...

Like
208
0
Thursday, 31 March 2016
VIETNAM: BUNGE LAPATA MWENYEKITI WA KWANZA MWANAMKE.
Local News

Bunge la Vietnam limepiga kura na kumpitisha Nguyen Thi Kim Ngan kuwa mwenyekiti wa bunge hilo kwa ushindi wa asilia 95.5% ya kura zilizopigwa. Ushindi huo wa Ngan, 61, unamfanya aingie kwenye rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kukamata nafasi hiyo ya uongozi katika taifa hilo. Kabla ya ushindi huo hapo awali Ngan alikuwa mkurugenzi wa idara ya fedha katika jimbo la nyumbani kwake la Ben...

Like
221
0
Thursday, 31 March 2016
UKRAINE: BUNGE LAHIDHINISHA HATUA YA KUJIUZULU KWA MWENDESHA MASHTAKA MKUU
Global News

BUNGE la Ukraine limeidhinisha hii leo hatua ya kujiuzulu kwa mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Viktor Shokin mtu ambaye amekuwa akionekana na nchi za magharibi zinazoiunga mkono Ukraine kama kizingiti katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Marekani imekuwa mara zote ikitaka pafanyike mageuzi kuanzia ngazi za juu katika ofisi hiyo ya mwendesha mashaka. Hata hivyo Wanaharakati wanaopinga rushwa wamekuwa wakisema kwamba ofisi ya mwendesha mashitaka huyo mkuu imekuwa na dhima muhimu katika kuyalinda maslahi ya wala rushwa na kuruhusu...

Like
220
0
Tuesday, 29 March 2016
ALIYEITEKA NDEGE YA MISRI AKAMATWA
Global News

RIPOTI zimesema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir amedai kuwa anahitaji kuongea na mkewe waliyetengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege. Rais wa Cyprus NicosAnastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi na kwamba wanahakikisha kuwa kila mtu anaachiliwa akiwa salama. Shirika la habari la Cyprus-CYBC limesema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake...

Like
185
0
Tuesday, 29 March 2016
MAKONDA AKABIDHIWA OFISI RASMI DARESALAAM
Local News

ALIYEKUWA mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick leo amemkabidhi rasmi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambapo amemuomba Mkuu huyo mpya wa mkoa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo afya na elimu. Akizungumza mbele ya maofisa na watendaji mbalimbali ambao wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia makabidhiano hayo Mheshimiwa Sadick amesema licha ya yeye kufanya kazi kwa mafanikio bado kuna changamoto ambazo anaamini kutokana na uzoefu alionao mkuu huyo wa mkoa...

Like
221
0
Tuesday, 29 March 2016
SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA AMABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI
Local News

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam na kufanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya kukiuka masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.   Hayo yamebainishwa leo na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili...

Like
224
0
Tuesday, 29 March 2016
MIKAKATI YA MOURINHO KUIBORESHA MAN UNTD
Global News

Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua nafasi ya Louis van Gaal. Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu. Kocha huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata. Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika...

Like
227
0
Tuesday, 29 March 2016
MAREKANI YAIFUNGUA IPHONE YA MLIPUAJI
Global News

WIZARA ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone, mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple. Wakili wa Marekani Eileen Decker amesema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa. Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye pamoja na mke wake wanatuhumiwa kuwaua watu kumi na nne kusini mwa California Desemba...

Like
225
0
Tuesday, 29 March 2016
NDEGE YA MISRI ILIYOTEKWA NYARA YATUA CYPRUS
Global News

NDEGE ya Misri iliyotekwa nyara imefanikiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus. Taarifa za uchunguzi kutoka kwenye ndege hiyo zimeeleza kuwa ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami. Msemaji wa shirika la ndege la Misri amenukuliwa akisema kwamba Watekaji hao waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus baada ya...

Like
233
0
Tuesday, 29 March 2016
MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ASIMAMISHWA KAZI
Local News

MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu John Aloyce amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kuisimamia halmashauri hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro kati ya madiwani na watendaji. Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Mbali na uamuzi huo Mtaka amefuta posho zote kwa wakuu wa Idara na vitengo katika halmashauri zote zilizopo mkoani hapo wanaoingia katika vikao vya madiwani...

Like
379
0
Tuesday, 29 March 2016
« Previous PageNext Page »