WAZIRI MKUU AAGIZA CAG KUKAGUA MAMLAKA YA BANDARI TPA
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali –CAG-aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akakague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.   Mheshimiwa Majaliwa ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji wao wa kazi.   Mbali na...

Like
240
0
Tuesday, 22 March 2016
TENISI: DJOKOVIC ATAKA WANAUME WALIPWE ZAIDI
Slider

Mchezaji nambari moja duniani katika mchezo wa tenisi Novak Djokovic amekosoa kutolewa kwa kiasi cha fedha sawa miongoni mwa wanaume na wanawake katika mchezo huo,akisema wanaume wanafaa kulipwa zaidi kwa kuwa wana mashabiki wengi. Baada ya kushinda taji la BNP Paribas huko India Wells,alitetea kiwango cha mashabiki kuangazia kiwango cha fedha kinachotolewa kwa wanamichezo wa jinsia zote mbili. Awali,mkurugenzi mkuu wa mashindano ya Indian Wells Ray Moore alisema kuwa michuano ya WTA inafanikishwa kutokana na kiwango cha mashabiki...

Like
240
0
Monday, 21 March 2016
MSHUKIA WA ALITAKA KUJILIPUA
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders amesema mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya kigaidi ya Paris, Salah Abdeslam, alikuwa anapanga kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels. Reynders amesema wamepata silaha nyingi, nzito na katika chunguzi za awali tangu kukamatwa kwa mshukiwa huyo, wamegundua mtandao mpya mjini Brussels unaohusishwa naye. Abdeslam anazuiwa katika gereza lenye ulinzi mkali huku akiwa amefunguliwa mashitaka ya mauaji ya kigaidi kwa kuhusika katika mashambulizi ya Novemba 13 mwaka jana mjini Paris...

Like
196
0
Monday, 21 March 2016
OBAMA AANZA ZIARA YA KIHISTORIA CUBA
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba, akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Taifa hilo katika kipindi cha miaka 88 iliyopita. Ziara hiyo ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa. Katika ziara yake Rais Obama atakutana na Rais wa Cuba Raul Castro Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa...

Like
212
0
Monday, 21 March 2016
TPA YATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA KISARAWE
Local News

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa Vitanda 20, Magodoro 20 na Shuka 100 kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.   Vitanda hivyo vya kisasa aina ya ‘Cardiac, mashuka pamoja na magodoro yake vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo ya wilaya vina thamani ya shilingi za kitanzania milioni 13.   Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi amesema msaada huo ni sehemu ya wajibu wa Mamlaka kuisaidia jamii ya Watanzania.  ...

Like
300
0
Monday, 21 March 2016
ZOEZI LA KUHESABU KURA LAENDELEA ZANZIBAR
Local News

ZOEZI la kuhesabu kura linaendelea visiwani Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana. Imeelezwa kwamba idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza kushiriki katika uchaguzi huo ambao ulisusiwa na baadhi ya vyama vikuu vya upinzani. Nchi nyingine za Afrika ambazo zimefanya Uchaguzi jana ni pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Niger na nchi ya Cape Verde ambapo tayari chama kikuu cha upinzani nchini humo MPD kimeshinda baada ya uchaguzi wa jana kwa zaidi ya asilimia 53 huku mkuu wa...

Like
226
0
Monday, 21 March 2016
HATIMAYE ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA HADHARANI
Slider

Kwa mara ya kwanza Manchester City yafuzu katika hatua hiyo ikikutana na vigogo kutoka nchini Ufaransa Paris St-Germain, Vita nyingine kali ni kati ya mabingwa wa Hispania Fc Barcelona dhidi ya majirani zao Atletico Madrid, huku Bayern Munich na Real Madrid wakipata mchekea. Wolfsburg (Germany) v Real Madrid (Spain) Bayern Munich (Germany) v Benfica (Portugal) Barcelona (Spain) v Atletico Madrid (Spain) Paris St-Germain (France) v Manchester City (England) Michezo hiyo inapigwa Tarehe 5 – 6 April na Marudiano ni Tarehe...

Like
283
0
Friday, 18 March 2016
BRAZIL: MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUTAWANYA WAANDAMANAJI
Local News

POLISI nchini Brazil wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwazuia waandamanaji kutoka makao makuu ya rais Dilma Roussef. Maelfu ya watu wanaotaka aachie madaraka waliandamana katika mji mkuu Brasilia. Wanamlaumu rais Roussef na chama chake cha workers party kwa ufisadi, lakini pia kulikuwa na maandamano ya kumpinga Roussef katika mji mkubwa zaidi nchini Brazil wa Sao...

Like
219
0
Friday, 18 March 2016
KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MAWILI YA MASAFA MAREFU
Global News

TAIFA la Korea Kaskazini limerusha makombora mawili ya masafa marefu katika bahari ya mashariki ya pwani yake, siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong-un kuagiza majaribio ya mabomu zaidi ya kinyuklia na silaha nyingine. Marekani imejibu kwa kutoa wito kwa Pyongyang kutozua wasiwasi katika eneo hilo ambao umekua juu tangu Korea Kaskazini ifanye jaribio la nne la mabomu yake ya kinyuklia mnamo mwezi Januari. Korea Kusini imeelezea jaribio hilo la hivi karibuni kama tishio kubwa la usalama na udhibiti...

Like
346
0
Friday, 18 March 2016
TASAF YAPATIWA DOLA MILIONI 665 KUNUSURU KAYA MASIKINI
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.   Mkataba huo ambao umetiwa saini jijini Dar es Salaam unawataka watendaji kuweka utaratibu ambao unaenda sambamba na Mpango wa utekelezaji bila kuingilia majukumu ya mamlaka ya Serikali katika utekelezaji wa TASAF wa kunusuru kaya masikini.   Akizungumzia mkataba huo mara baada ya kusaini kwa niaba...

Like
213
0
Friday, 18 March 2016
RAIS MAGUFULI AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa Hospitali ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi-CCM-kwa wananchi wa Jimbo hilo. Akikabidhi gari hilo leo Ikulu Jijini Dar es salaam kwa mbunge wa Jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Rais ikiwa ni kuitikia wito wa...

Like
306
0
Friday, 18 March 2016
« Previous PageNext Page »