JWTZ YAKANUSHA KUPELEKA MAJESHI ZANZIBAR
Local News

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi wa marudio unaotarajia kufanyika Machi 20 mwaka huu.   Jeshi hilo limesema kuwa Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma kwani JWTZ lina Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa Taifa hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale...

Like
266
0
Thursday, 17 March 2016
WZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 2 CHATO
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.   Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, bwana Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Dioniz Mutayoba.   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana usiku alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano...

Like
362
0
Thursday, 17 March 2016
TRUMP APETA MAJIMBO MUHIMU MAREKANI
Global News

DONALD TRUMP amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo katika majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida.   Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.Hata hivyo ameshindwa na John Kasich katika jimbo la Ohio.   Mgombea anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North...

Like
252
0
Wednesday, 16 March 2016
MCHAKATO WA KUMALIZA KERO YA MIUNDOMBINU WAANZA KUFANYIWA KAZI TANDIKA
Local News

DIWANI wa kata ya Tandika Ramadhani Litumangiza amesema kuwa mchakato wa kuimaliza kero kubwa ya miundombinu ya barabara za ndani ya mtaa huo ambazo zimekuwa na mashimo na kutopitika kipindi cha mvua umekamilika na kuanza kufanyiwa kazi hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Tandika jijini Dar es salaam, Diwani Ramadhani amesema kuwa kumekuwa na kero hiyo ambapo kipindi cha mvua maji hujaa kwenye madimbwi yaliyopo barabarani na kuingia kwenye nyumba za watu. Ameongeza kuwa tayari amefanikiwa kupata...

Like
303
0
Wednesday, 16 March 2016
SERIKALI IMEOMBWA KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA AFYA KWA WATU WENYE ULEMAVU
Local News

SERIKALI imeombwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya kwa watu wenye ulemavu na mahitaji maalum kwenye hospitali zake. Rai hiyo nimetolewa jijini Dares salaam na Katibu Mkuu wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi –Albinisim, bwana Gaston Mcheka alipokuwa akizungumza na kituo hiki kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo wanapokwenda kupata huduma hizo. Mcheka amesema, kumekuwa na unyanyapaa mkubwa kwa watendaji wa hospitali hizo na kuonekana kutokuwa na thamani ya kuhudumiwa kwa haraka suala linalowafanya wajione...

Like
237
0
Wednesday, 16 March 2016
UEFA: MAN CITY YATINGA ROBO FAINALI
Slider

Manchester City wamefika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza licha ya kutoka sare na Dynamo Kiev mechi ya marudiano. City, waliokuwa mbele 3-1 kutokana na ushindi wa mechi ya kwanza, walidhibiti mechi ingawa waliwapoteza mabeki Vincent Kompany na Nicolas Otamendi kutokana na majeraha mapema. Kipindi cha kwanza hakuna aliyetishia mwenzake lakini kipindi cha pili Jesus Navas aligonga mlingoti kwa kombora la chini naye Yaya Toure akatoa kombora ambalo lilitua mikononi mwa kipa. Manuel Pellegrini, atakayeondoka mwisho...

Like
201
0
Wednesday, 16 March 2016
PUTIN AAGIZA MAJESHI YA URUSI KUONDOKA SYRIA
Global News

RAIS wa Urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa wanajeshi wake waliopo Syria kurejea nyumbani haraka kwa sababu tayari wametekeleza asilimia kubwa ya malengo yao. Tangazo lake hilo limewaacha wachambuzi wengi wakiwa na mshangao kwani hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kwa tukio kama hilo. Aidha Putin ametangaza hilo katika siku ambayo mazungumzo ya amani yameanza upya mjini Geneva Uswisi....

Like
239
0
Tuesday, 15 March 2016
KOREA KASKAZINI YATANGAZA KUFANYA JARIBIO LA NYUKLIA
Global News

KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametangaza kwamba Taifa hilo litafanya majaribio ya silaha zake za nyuklia na makombora ya masafa marefu hivi karibuni. Kim Jong-un ametoa Tangazo lake alipokuwa akiongoza maonesho ya teknolojia ambayo inahitajika kuwezesha kombora lenye kilipuzi cha nyuklia kuingia tena ardhini baada ya kurushwa anga za juu. Shirika hilo limemnukuu kiongozi huyo akisema kuwa majaribio hayo yatafanyika na yataisaidia Korea Kaskazini kujiimarisha katika utekelezaji wa mashambulio ya...

Like
228
0
Tuesday, 15 March 2016
KAGERA :AFISA MIFUGO ANUSURIKA KUFUKUZWA KAZI
Local News

AFISA MIFUGO wa kata ya Kakunyu, wilayani Misenyi mkoani Kagera, Eric Kagoro amenusurika kufukuzwa kazi kwenye mkutano wa hadhara kutokana na sakata la kuruhusu ng’ombe 291 kulishwa kwenye ranchi ya mifugo ya Misenyi. Tukio hilo limetokea jana baada ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kuhoji juu ya malalamiko aliyoyapata kutoka kwa wananchi kuwa Afisa huyo ndiye aliyeruhusu mifugo hao kuingia kwenye eneo hilo. Katika mkutano huo Waziri Mkuu amewaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina...

Like
375
0
Tuesday, 15 March 2016
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA RASMI WAKUU WA MIKOA 26
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John pombe Magufuli amewaapisha rasmi wakuu wa mikoa 26 wa Tanzania Bara aliowateua machi 13 mwaka huu. Hafla ya kuwaapisha wakuu hao wa mikoa imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan. Baadhi ya wakuu wa mikoa walioapishwa leo ni pamoja na Mheshimiwa Said Meck Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Paul Makonda mkuu wa mkoa...

Like
198
0
Tuesday, 15 March 2016
ANGELA MERKEL ACHEMKA UCHAGUZI WA MAJIMBO
Global News

CHAMA cha Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeshindwa katika uchaguzi wa majimbo, matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi yanaonesha. Chama cha AfD kinachowapinga wahamiaji, kimeimarika kwa kiwango kikubwa katika majimbo yote matatu. Uchaguzi huo ulitazamwa na wengi kama kigezo cha uungwaji mkono wa sera ya kansela Merkel ya kuwapokea wakimbizi, ambapo zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja waliingia Ujerumani mwaka 2015....

Like
224
0
Monday, 14 March 2016
« Previous PageNext Page »