JAMII IMETAKIWA KUUNGA MKONO UKUZAJI WA VIPAWA
Local News

JAMII nchini imetakiwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanya na baadhi ya taasisi zinazo jihusisha na utoaji wa ujuzi na uendelezaji wa vipawa vya watoto na vijana ili kujenga jamii yenye tabia ya kujitegemea . Hayo yamebainishwa na Mkude Kilosa ambaye ni  mkurugenzi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto na vijana cha baba watoto kilichopo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na efm  juu ya maandalizi ya tamasha la wazi la sarakasi tamasha lililolenga kukuza na kuendeleza ujuzi wa vijana katika...

Like
198
0
Friday, 26 February 2016
WFP LATOA MSAADA DEIR EL-ZOUR
Global News

MKUU wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utoaji wa misaada ya kibinaadamu, Stephen O’Brien, amesema shirika la Mpango wa Chakula duniani, WFP, limedondosha chakula kutoka angani katika mji wa Deir el-Zour, ambao umekuwa ukizingirwa na kundi la Dola la Kiislamu. O’Brien ameliambia baraza la usalama la umoja huo mjini New York kwamba tani 21 za msaada zilidondoshwa. Hata hivyo msemaji wa WFP Bettina Luescher amesema katika taarifa yake kwamba operesheni nzima ilikabiliwa na changamoto za...

Like
197
0
Thursday, 25 February 2016
WANAJESHI 180 WA KENYA WALIUAWA NA AL-SHABAB
Global News

RAIS wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ametoa maelezo kuhusu idadi ya wanajeshi wa Kenya waliofariki kufuatia shambulio la al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde mwezi uliopita.   Rais huyo ametoa idadi hiyo kuwa kati ya wanajeshi 180 na 200 katika mahojiano na runinga moja ya Somali ,Cable TV.   Wapiganaji hao wa al-Shabab wamesema kuwa wanajeshi 100 walifariki na Kenya bado  haijatoa idadi yoyote ya wanajeshi wake...

Like
191
0
Thursday, 25 February 2016
SERIKALI YATAKIWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA UBORA WA ELIMU
Local News

SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kuwekeza zaidi katika ubora wa elimu na sio katika kutanua upatikanaji na nafasi ya elimu ili kutekeleza sera ya Elimu bure kwa Shule za Serikali kwa kuwa tafiti zinaonesha kuwa kiwango cha ufaulu katika miaka 10 iliyopita kimeshuka katika Shule za Msingi na Sekondari licha ya mfumo huo kutumika katika elimu ya msingi.   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti iliyotolewa na Twaweza kuhusu maoni ya Wananchi juu...

Like
222
0
Thursday, 25 February 2016
TANZANIA NA ZAMBIA ZIMETAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO
Local News

WIZARA ya Mambo ya Nje ya Nchi Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kanda na Kimataifa Nchini,  imezitaka  Nchi za Tanzania na Zambia kuongeza ushirikiano ili kuleta mafanikio ya pamoja katika Sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na Biashara, Uchumi, Mawasiliano, Elimu, Utamaduni, Utalii,Kilimo pamoja na maswala ya Tekinolojia.   Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ramadhan Mwinyi alipozungumza  katika Ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Tume  ya  Kudumu ya Pamoja -JPC- kati ya Tanzania na Zambia ambapo amesema...

Like
177
0
Thursday, 25 February 2016
OBAMA ATOA MSUKUMO WA MWISHO WA KUFUNGWA KWA GEREZA LA GUANTANAMO BAY
Global News

RAIS  Barack Obama  wa  Marekani  ameanzisha  msukumo wa  mwisho leo kulishawishi  baraza  la  Congress kulifunga  gereza  la  kijeshi  la Guantanamo Bay nchini Cuba. Rais Obama  amelitaka  baraza  la  Congress kulijadili  kwa kina  pendekezo  lake na  kuongeza  kwamba  hataki kuliacha  suala  hilo  kwa  mrithi  wake mwezi ...

Like
262
0
Wednesday, 24 February 2016
SERIKALI YAITAKA KAMPUNI YA KADCO KUIMARISHA ULINZI KIA
Local News

SERIKALI imeitaka kampuni ya KADCO inayoendesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro-KIA, kuongeza mapato na kuimarisha ulinzi ili kulinda hadhi ya uwanja huo, kuchangia pato la serikali na kudhibiti hujuma dhidi ya watu wasio waaminifu. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo wakati akikagua utendaji na mradi wa ujenzi wa njia za kurukia ndege unaondelea katika uwanja...

Like
287
0
Wednesday, 24 February 2016
MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA PROGRAM MAALUM YA MWANAMKE NA WAKATI UJAO
Local News

MAKAMU wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua program maalumu ya mwanamke na wakati ujao ambayo itawajengea wanawake uwezo katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na Kampuni mbalimbali. Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye hote ya Hayatt Regency jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo kutoka nchini za Kenya na Uganda pamoja na wengine kutoka Ulaya na Asia, Mheshimiwa Suluhu amesema kuwa, wanawake ni watendaji wazuri na wanamaamuzi sahihi katika uongozi...

Like
276
0
Wednesday, 24 February 2016
CRISTIANO RONALDO NDIO MWANAMICHEZO MWENYE WAFUASI WENGI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Slider

Cristiano Ronaldo aweka rekodi ya kuwa mwanamichezo wa kwanza kuwa na followers wengi kwenye mitandao ya kijamii. Nyota huyu wa Real Madrid ana jumla ya watu Milioni 200 wanaoperuzi kwenye kurasa zake. Hii ndio number ya followers kwenye akaunti za mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram Twitter 40.7M, Instagram 49.6M wakati Facebook ni 109.7M Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na tovuti ya...

Like
226
0
Wednesday, 24 February 2016
DONALD TRUMP ASHINDA KATIKA JIMBO LA NEVADA
Global News

MGOMBEA wa urais wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini Marekani, na hivyo basi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho. Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini. Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya...

Like
166
0
Wednesday, 24 February 2016
NEPAL: NDEGE YA ABIRIA YATOWEKA
Global News

NDEGE ndogo iliyowabeba abiria 21 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal. Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo. Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Tara Airlines imeanguka....

Like
173
0
Wednesday, 24 February 2016
« Previous PageNext Page »