SYRIA: MATAIFA YAAFIKIANA KUSITISHA MAPIGANO
Global News

MATAIFA yenye ushawishi duniani yameafikiana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano nchini Syria ambao utaanza kutekelezwa katika kipindi cha wiki moja ijayo. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo nchini Ujerumani. Mwafaka huo hata hivyo hautahusisha makundi ya kijihadi ya Islamic State (IS) na al-Nusra Front. Aidha, Mawaziri wa mataifa wanachama wa Kundi la Kimataifa la Kusaidia Syria pia wamekubaliana kuharakisha na kuongeza juhudi za kutoa...

Like
173
0
Friday, 12 February 2016
ICC: HATMA YA RUTO KUFAHAMIKA LEO
Global News

MAHAKAMA ya jinai ya kimataifa -ICC leo inatarajiwa kutoa uamuzi ambao huenda ukakuwa na athari kwa kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto. Bwana Ruto na mushtakiwa mwenzake, mwana Habari, Joshua Arap Sang wameshitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Mashtaka kama hayo yaliyomkabili rais Uhuru Kenyatta yalifutiliwa mbali na mwendesha mkuu wa mashataka ya ICC, Fatou Bensouda kwa ukosefu wa...

Like
240
0
Friday, 12 February 2016
KIGWANGALLA: TUTAENDELEA KUTUMBUA MAJIPU
Local News

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya ,bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya  taifa.   Dokta Kigwangala ameyasema hayo  wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea  wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo Kuu la Tabora  na baadae kwenye...

Like
182
0
Friday, 12 February 2016
TRA YANASA SHEHENA KUBWA YA BIDHAA ZA MAGENDO
Local News

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali ya Ukanda  wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na mipakani.   Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo katika mahojiano maalum yaliyofanyika  ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.   Amesema kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi milioni kumi kutoka katika bidhaa zilizokuwa...

Like
253
0
Friday, 12 February 2016
RONALDO AONYESHA NIA YA KUBAKI REAL MADRID
Slider

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema hataki kuondoka klabuni hapo kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka 2018. Mreno huyo mwenye miaka 31 amekua akihusishwa na kurudi kujiunga na timu yake ya zamani ya Manchester United, ambayo ilimuuza mwaka 2008 au Paris St-Germain, ya Ufaransa. “Nataka kubakia hapa kwa miaka miwili zaidi, miaka miwili ninayozungumzia itanichukua mpaka mwisho wa maktaba wangu, “alinukuliwa mchezaji huyo. Ronaldo alizungumza hayo wakati ya ghafla ya uchukuaji tuzo ya Pichichi, amabpo alishinda tuzo hiyo...

Like
163
0
Tuesday, 09 February 2016
MAPENDEKEZO YATOLEWA NEYMAR ASHTAKIWE
Slider

Waendesha mashtaka nchini Brazil wamependekeza kwamba nyota wa timu ya Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake hadi Barcelona. Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini. Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai hayo dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia 2006.Madai hayo ni tofauti na yale ya kesi iliosikizwa siku ya Jumanne nchini Uhispania. Neymar...

Like
185
0
Wednesday, 03 February 2016
AMIR KHAN KUPAMBANA NA ALVAREZ
Slider

Bondia mwingereza Amir khan anatarajia kupigana na bondia kutoka Mexico sauli Alvarez kuwania mkanda wa WBC katika uzito wa kati mnamo mei saba mjini Las Vegas. Khan mwenye miaka 29, ambaye ni bingwa wa dunia katika uzito wa welter hajapigana tangu apigwe na Chris Algieri mjini New York mwezi Mei. Kwa upande wake Alvarez mwenye miaka 25, amewahi kumpiga bondia Miguel Cotto kwa pointi mjini Las Vegas mwezi Novemba. Mpaka sasa amepoteza pambano mara moja huku akishinda mara 46 katika...

Like
230
0
Wednesday, 03 February 2016
JENERALI SEJUSA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Global News

JENERALI mwenye utata nchini Uganda David Sejusa amewasili katika mahakama moja ya kijeshi katika mji mkuu wa Kampala nchini Uganda tayari kujibu mashitaka yanayomkabili ambayo hata hivyo bado hayajawekwa hadharani. Siku ya jumatatu chombo cha habari cha Bloomberg kilimnukuu msemaji wa serikali Ofwono Opondo akisema kuwa Uganda inachunguza ripoti zinazomuhusisha jenerali mtoro David Sejusa na makundi yenye mipango ya kuzua ghasia. Jenerali Sejusa aliwekwa katika kifungo cha nyumbani siku ya jumapili mjini...

Like
166
0
Tuesday, 02 February 2016
UGANDA YAZINDUA BASI LINALOTUMIA UMEME WA JUA
Global News

UGANDA imefanikiwa kuzindua rasmi basi linalotumia nguvu ya umeme wa jua ambalo limedaiwa kuwa watengezaji wake wanatoka nchini humo na ni la kwanza kama hilo kutengenezwa barani Afrika. Basi hilo la kielektroniki aina ya Kayoola linalomilikiwa na kampuni ya Kiira Motors limeonyeshwa kwa waganda katika uwanja wa Uganda mjini Kampala. Mojawapo ya betri zake zinaweza kuwekwa chaji na vibamba vya umeme wa jua katika paa la nyumba ambazo huongeza kasi ya gari hilo hadi kilomita 80 kwa saa....

Like
191
0
Tuesday, 02 February 2016
WANANCHI WATAKIWA KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA CHANJO
Local News

WIZARA ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imewataka wananchi kuhakikisha wana wapeleka watoto wote kwenye vituo husika vya Afya ili wapatiwe Chanjo na kinga ya kichocho ili kuwanusuru na ugonjwa wa kichocho. Rai hiyo imetolewa keo jijini Dar es salaamu na mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Pendo Mwingira ambapo amesema wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO limeaamua kutoa chanjo ya kumkinga mtoto dhidi ya Ugonjwa wa kichocho kwa kuwa huwaathiri zaidi watoto....

Like
188
0
Tuesday, 02 February 2016
SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI
Local News

SERIKALI imejipanga kuhakikisha inaboresha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchini ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa.   Akijibu swali la Mheshimiwa Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF), leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya masikini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika.   Aidha Mheshimiwa Kairuki amesema kuwa...

Like
170
0
Tuesday, 02 February 2016
« Previous PageNext Page »