EFM RADIO, YAKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA MADARASA YA SEKONDARI-KATA YA KIMARA- KINONDONI.
Local News

WILAYA ya Kinondoni kupitia Mkuu wa Wilaya hiyo inatarajia kuongeza shule za Sekondari ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika Wilaya hiyo. Efm Radio 93.7 katika kuunga mkono juhudi hizo za Serikali imeahidi kujenga madarasa mawili . Mkuu wa Vipindi vya 93.7 efm Dickison Ponela akipokea mchoro wa madarasa, kutoka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana, Rogers J. Shemwelekwa Katikati ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo, Scholastica Mazula na Pembeni kushoto ni Injinia wa Wilaya hiyo Bwana Brighton. Mhariri...

Like
500
0
Thursday, 21 January 2016
IRAN YAKAMATA BOTI 2 ZA DORIA ZA MAREKANI
Global News

BOTI mbili za doria za Marekani zikiwa na wafanyakazi 10 zimekamatwa nchini Iran.   Maafisa wa Marekani wamesema boti hizo zilikuwa katika mazoezi kati ya Kuwait na Bahrain kwenye eneo la Ghuba, baada ya moja wapo kupata matatizo ya kiufundi na kupoteza mwelekeo hadi katika maji ya Iran.   Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani John Kery amewasiliana na mwenziye wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amemhakikishia kwamba wanamaji wa boti hiyo watarudishwa mara...

Like
227
0
Wednesday, 13 January 2016
SUDANI KUSINI: NUSU YA WATOTO WAKATISHA MASOMO
Global News

  SHIRIKA linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto walioko Sudan kusini hawako shule.   Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani.   Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani na kwamba tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane...

Like
183
0
Wednesday, 13 January 2016
WAFANYABIASHARA TEGETA KWA NDEFU WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA ENEO MAALUM LA SOKO
Local News

WAFANYABIASHARA  wa soko lisilo rasmi lililopo tegeta kwa ndevu  Jijini  Dar es salaam wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum la kufanyia biashara zao kutokana soko la nyuki  lililotengwa  kuwa finyu  hali inayosababisha wao kuendelea kuwepo sokoni hapo.   Wakizungumza na efm Jijini  Dar es salaam Wafanya Biashara hao wamesema kuwa  kipinndi cha nyuma eneo hilo lilikuwa lipo chini ya serikali  ya mtaa ambapo kwa sasa linamilikiwa na mtu binafsi ambae ndie amewapangisha.   Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Soko hilo...

Like
326
0
Wednesday, 13 January 2016
MAKAA YA MAWE KUZALISHA UMEME TANZANIA
Local News

  SERIKALI imesema  itahakikisha  inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini.   Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea  Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia Kati ya Kampuni ya  TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC.   Mgodi huo  upo katika Wilaya ya  Mbinga mkoani...

Like
257
0
Wednesday, 13 January 2016
GARISSA: WANAFUNZI WAREJEA CHUONI
Local News

WANAFUNZI wamerejea tena katika Chuo Kikuu cha Garissa na kuanza masomo miezi tisa baada ya chuo hicho kufungwa kutokana na shambulio la al-Shabab, Nchini Kenya. Serikali imesema imeweka usalama wa kutosha kuhakikisha kundi hilo kutoka Somalia haliwezi likashambulia tena, lakini licha ya hakikisho kutoka kwa maafisa wa usalama, ni wanafunzi wachache pekee waliorejea chuoni. Takriban wanafunzi 800 wa kufadhiliwa na serikali, waliokuwa wakisomea katika chuo hicho kabla ya shambulio kutokea, walihamishiwa chuo kikuu cha Moi mjini...

Like
178
0
Monday, 11 January 2016
CUF YAGOMA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR
Local News

WAKATI kesho ni maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi, Chama cha Wananchi –CUF, kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar. Taarifa ya chama hicho ambayo imesomwa leo na aliyekuwa mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana,  Maalim Seif  imeeleza kuwa hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi  huo kurudiwa. Taarifa hiyo imeonyesha kutoa mapendekezo ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim...

Like
213
0
Monday, 11 January 2016
13,491 WAGUNDULIKA KUWA NA KIPINDUPINDU
Local News

JUMLA ya Watu elfu 13,491 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu tokea kuanza kwa ugonjwa huo Agosti 15 Mwaka jana na kuwa kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huo.   Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ahmis Kigwangala, wiki iliyoaanza tarehe 4 hadi leo 11 Januari,  kumekuwa na jumla ya Wagonjwa 615 walioripotiwa nchini na vifo 3 hali inayoonyesha kuwa hali ya kipindupindu nchini bado sio nzuri....

Like
210
0
Monday, 11 January 2016
RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA SUMAYE HOSPITALI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli, amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye leo, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.   Mheshimiwa Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.  ...

Like
338
0
Monday, 11 January 2016
UFARANSA YAWAKUMBUKA WALIOUAWA KIGAIDI PARIS
Global News

RAIS wa Ufaransa Francois Hollande na Meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo waliweka bango la taarifa katika eneo la Place de la Republique kuwakumbuka watu 147 waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris mnamo mwezi Novemba mwaka jana.   Rais Hollande aliungana na viongozi wengine na maelfu ya raia kuwakumbuka wahanga hao wa mashambulizi ya kigaidi ambayo kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS lilidai kuhusika.   Wiki nzima iliyopita, Ufaransa...

Like
172
0
Monday, 11 January 2016
SYRIA: UN YATOA MSAADA MADAYA
Global News

UMOJA wa mataifa umesema kuwa misafara ya magari iliyobeba chakula cha mwezi mzima na dawa leo umeanza kuelekea nchini Syria katika mji wa Madaya eneo ambalo limeathiriwa na njaa ambapo baadhi yao wamekufa kutoka na hali hiyo.   Watu zaidi ya elfu 40 wamezuiwa na serikali kutoka katika maeneo hayo na hawajahi kupokea msaada wa chakula tangu mwezi Oktoba mwaka jana.   UN wanasema kuwa wanaushahidi kwamba baadhi wamekufa kwa njaa katika mji huo wa Madaya nchini Syria kutokana na...

Like
187
0
Monday, 11 January 2016
« Previous PageNext Page »