KATIKA kupunguza tatizo la watoto wengi wanaomaliza darasa la saba kushindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kutokana na uhaba wa Madarasa wilayani Kinondoni , Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda leo ameweka mawe ya msingi ya ujenzi wa shule za Sekondari Mbezi Juu na shule ya Sekondari Mzimuni zinazojengwa katika manispaa ya Kinondoni. Akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na wananchi wakati akiweka mawe hayo ya msingi Makonda amesema hii ni sehemu yamkakati wa Manispaa hiyo kujenga shule za...
SERIKALI imesema imejidhatiti kuwalinda wananchi kwa kuzuia athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula kisicho salama kote nchini. Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza ameyasema hayo na kufafanua kuwa uchafuzi wa chakula hufanya chakula kisiwe salama na hivyo kusababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu na hata vifo kwa mlaji pamoja na athari za...
Baada ya kufnya vizuri na track yake ya kwanza kama solo artist, Dream ameachia wimbo mpya unaweza kuusikiliza na kuupakua hapa Wimbo umetayarishwa na Abbah katika studio za Vipaji TZ pakua...
JESHI la Israel limesema kwa Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kujaribu kuwachoma visu wanajeshi wa Israel katika matukio mawili tofauti eneo la Ukingo wa Magharibi. Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali na mwingine aliuawa karibu na Hebron lakini hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa. Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo...
RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso na dhiki ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili. Rais Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika kufanikisha maridhiano nchini humo. Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa chama tawala cha SPLM. Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya...
BALOZI wa Uingereza nchini ameahidi kuisaidia Halmashauri ya kinondoni katika kutatua kero ikiwemo kero ya mafuriko pamoja na kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ,sekta ya afya na michezo. Hayo yamebainishwa jijini Dar es alaamu na mkuu wa wilaya ya kinondoni PAUL MAKONDA mara baada ya kumaliza mazungumzo na balozi huyo, DIANA MELYROSE ambapo amesema kutokana na kuwepo na changamoto mbalimbali katika manispaa ya kinondoni manispaa hiyo imekuwa na mazungumzo na baadhi ya wadau wa halmashauri ya kinondoni wakiwemo...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku. Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa...
Kampuni Ya Quality Media Group Yanunua Gazeti La Jambo Leo Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambao ni wachapishaji wa Gazeti la kila siku la Jambo Leo imenunuliwa na Kampuni ya Quality Media Group ambayo ni kampuni tanzu ya Quality Group Limited,ununuzi umeanza December 31 na unategemea kukamilika February 01. Kampuni ya Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la Jambo Leo na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016...
Nyota ya Tanzania inayowika TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika. Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani. Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria. Samatta, kijana anayevumisha soka ya Tanzania Timu...
WATU 70 wameuwawa wakati lori lililokuwa limewekewa miripuko kuripuka katika kambi ya polisi Kaskazini Magharibi ya Libya katika mji wa pwani wa Zliten. Watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga, ambalo lilishambulia kundi la maafisa wa polisi waliokuwa wamekusanyika jana katika kambi . Kwa mujibu wa watu walioshuhudia, lori hilo lililokuwa na miripuko liligonga katika lango la kambi hiyo ambayo inatumiwa kuwapa ...
HATIMAYE, RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamefikia makubaliano ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kuhusiana na muundo wa serikali ya mpito. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali inaruhusiwa kuteua mawaziri 16, ambapo upande wa waasi wanaruhusiwa kuteua mawaziri 10. Serikali ya mpito iliyokubaliwa itakuwa madarakani kwa miaka 3 kabla ya uchaguzi mpya kufanyika. Sudan Kusini imekumbwa na vita vya ...