WANANCHI wa Kijiji cha Itamboleo Kata ya Chimala Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamemtaka Mkugunzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kumchukulia hatua za nidhamu Mtendaji wa Kijiji Julius Mwagala kwa ubadhilifu wa fedha za kijiji. Mwenyekiti wa Kijiji cha Itamboleo SAMWEL KAGANGA amesema kuwa Mwagala amekula shilingi laki 9 zilizochangwa na wananchi mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo ya Kijiji. Hata hivyo inaelezwa kuwa, mtendaji huyo hajafika kazini tangu mwezi March mwaka jana ambapo kazi zake zimekuwa zikifanywa...
KATIKA kuhakikisha agizo la serikali la kufikisha huduma ya maji safi kwa wakazi zaidi ya milioni nne wa mkoa wa Dar es alaamu na mikoa ya jirani, mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Dar es alaamu- DAWASCO, limeanzisha zoezi maalumu kwa ajili ya kuwaunganisha wakazi hao na huduma hiyo. Afisa uhusiano wa Dawasco EVERLASTINGI LYARO, amesema kuwa zoezi hilo limeanza rasmi tangu januari mosi mwaka huu na limegawanyika katika awamu kuu nee. LYARO amebainisha kuwa...
WAFUNGWA wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009. Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa...
MZOZO wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran unazidi kufukuta, huku Iran ikiitaka Saudi Arabia kuachana na msimamo wake wa makabiliano. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, ameitaka Saudi Arabia kuacha kuchochea wasiwasi na kujibu hatua zake za karibuni, ambazo zilisababisha mkwamo...
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa, George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Dennis Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara. Kutokana na hali hiyo Waziri ameelekeza Mkurugenzi huyo wa Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein ametaka tofauti za kisiasa zilizopo Visiwani humo zisitumike kuvuruga amani na utulivu ambayo ndiyo siri kubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika visiwa vya Unguja na Pemba. Dokta Shein ambaye alikuwa akizungumza na wananchi wa Wete waliokwenda kumsalimia mara baada ya kukagua ujenzi wa soko na Ofisi ya Baraza la Mji wa Wete, amesema kuwa suala la amani halina mbadala huku akiahidi kuendelea kuisimamia amani ya Zanzibar na...
RAIS Alassane Ouattara wa Ivory Coast amekubali kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Serikali yake. Akituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, Outtarra amesema waziri mkuu aliwasilisha hati ya kujiuzulu na ile ya serikali naye akairidhia. Ouattara, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 74, aliyewahi kulitumikia shirika la fedha la kimataifa na amechaguliwa kwa muhula wa pili wa miaka mitano kama rais, mwezi Oktoba mwaka...
SIKU moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la haidrojeni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo. Hata hivyo baadhi ya Wataalamu wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika mwongo mmoja, wakisema huenda lisiwe la haidrojeni kutokana na mlipuko uliotokea. Bomu la hydrojeni ni moja ya mabomu hatari ya jamii ya atomiki au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu...
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania- TTB, kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN na BBC kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala na matangazo ya utalii katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani. Waziri Maghembe amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watalii nchini. Waziri Maghembe ameyasema hayo alipotembelea Bodi ya Utalii...
WAZIRI wa kilimo,mifugo na uvuvi mheshimiwa Mwigulu Nchemba amewasimamisha viongozi wa vyama vya ushirika vya zao la tumbaku mkoani Iringa. Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo, Mheshimiwa Mwigulu amemuagiza mrajisi wa mkoa kuivunja bodi hiyo na kuwachunguza viongozi wa vyama hivyo. Aidha, ameiomba serikali ya mkoa kufuatilia na kutathimini ubadhirifu uliofanywa na viongozi hao na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo...
MAHAKAMA moja ya Kiislamu nchini Nigeria imemhukumu kifo mhubiri anayetuhumiwa kukufuru kwa kumtukana Mtume Muhammad. Abdul Inyass amehukumiwa katika kikao cha faragha cha mahakama katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria. Afisa wa mashtaka Lamido Abba Soron-Dinki ameliambia shirika la AFP kuwa Kikao hicho kimefanyika faraghani kuzuia “fujo kutoka kwa umma” sawa na ilivyoshuhudiwa wakati wa kikao cha...