KOREA KASKAZINI imesema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni. Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia. Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu....
JUMLA ya shilingi trilioni 1.4 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015. Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi. Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Ernest Mangu kufuatia kifo cha msaidizi wake Inspekta – Gerald Ryoba aliyepoteza maisha katika ajali ya kusombwa na mafuriko ya maji wakati akikatiza katika eneo la Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Katika ajali hiyo iliyotokea Januari 3 mwaka huu, Inspekta Ryoba akiwa na Mkewe na watoto wake wawili, pamoja na watu wengine wawili walikuwa wakisafiri...
RAIS wa Marekani Barack Obama ametangaza hatua kadhaa zinazonuwiwa kukabiliana na matumizi mabaya ya silaha nchini humo, zikiwemo upatikanaji wa lazima wa leseni kwa wauzaji silaha na kufanya ukaguzi wa historia za wateja. Obama ametangaza hatua hizo katika ikulu ya White House akiwa amezungukwa na manusura wa mashambulizi ya silaha yanayouwa karibu Wamarekani 30,000 kila mwaka. Hata hivyo Obama amekiri kuwa hatua hizo alizozipitisha mwenyewe bila kulishirikisha bunge la Congress, hazitomaliza kabisa tatizo la matumizi mabaya ya...
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa mzozo unaozidi kufukuta kati ya Riyadh na Tehran hautaathiri mazungumzo ya amani ya Syria. Taarifa yake ilikuja wakati Kuwait nayo ikimrudisha balozi wake kutoka Iran, kuiunga mkono Saudi Arabia. Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine kadhaa ya Kiarabu, yamechukuwa hatua dhidi ya Iran, baada ya ubalozi wake kushambuliwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wanapinga kuuawa kwa kiongozi wa Kishia na mkosoaji wa serikali ya Saudi Sheikh Nimr...
SERIKALI wilayani Pangani imewapa miezi mitatu baadhi ya watu waliohodhi viwanja vikiwemo vile vilivyopo pembezoni mwa bahari ya hindi kuviendeleza la sivyo haitasita kuwanyang’anya kwa mujibu wa sheria ili kuendeleza mji wa pangani ambao sehemu kubwa ya makao makuu ya wilaya imezungukwa na mapori. Akizungumza na efm kuhusu baadhi ya wafanyabiashara kuhodhi maeneo kwa makusudi kwa lengo la kuyafanyia biashara, mkuu wa wilaya ya pangani Regina Chonjo amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU. Alikuwa akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini. Waziri...
Kuwait imetangaza kwamba inamuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi. Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi. Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata....
MAAFISA wa usalama nchini Kenya wanawasaka washukiwa wanne wa ugaidi ambao wanadaiwa kukwepa msako wa polisi katika nyumba moja Mombasa. Polisi walipata bunduki mbili na vilipuzi baada ya kuvamia nyumba iliyokuwa ikitumiwa na wanne hao Jumatatu. Kamishna wa jimbo la Mombasa Nelson Marwa anasema bunduki moja iliyopatikana ilitumiwa kumuua afisa wa polisi mjini humo mwaka...
VIONGOZI wa Mkoa wa Geita wametakiwa wasiwaonee aibu kuwafungia wafanyabiashara wasiofuata kanuni za usafi wa mazingira na hivyo kupelekea mlipuko wa kipindupindu. Hayo yamesema na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kambi ya wagonjwa ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya Nyankumbuli mjini Geita. Waziri Ummy amesema mlipuko wa kipindupindu upo hivyo kuwafumbia macho wale ambao wanafanya biashara katika mazingira yasiyo safi na salama lazima watu hao wafungiwe. ...
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene, amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam –DART, uteuzi ambao umeanzia jana. Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria Mlambo aliyesimamishwa tarehe...