UMOJA wa Afrika umeamua utapeleka ujumbe maalum nchini Burundi kujaribu kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuridhia jeshi la kulinda amani baada ya rais Nkurunzinza kuipinga hatua hiyo. Taarifa hizo zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika baada ya kumalizika mkutano wa kilele wa Umoja huo hapo jana. Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka nchi za Magharibi aliyefuatilia mkutano wa jana ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba viongozi wa Umoja wa Afrika waliokutana kwa...
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) leo linafanya mkutano wa dharura kujadili kuenea kwa virusi vya Zika. Mkutano huo mjini unaofanyika Geneva utajadili iwapo mlipuko wa virusi hivyo unafaa kutangazwa kuwa dharura ya kimataifa. Katika matukio mengi, watu walioambukizwa virusi hivyo vya Zika huwa hawaonyeshi dalili zozote, lakini virusi hivyo vinadaiwa kusababisha maelfu ya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo Amerika...
WIZARA ya Fedha na Mipango leo imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa maendeleo ya Taifa pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 unaolenga utekelezwaji wa vipaumbele mbalimbali vya kuleta maendeleo. Akiwasilisha mapendekezo ya mpango na mwongozo huo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango dokta Philip Mpango amesema kuwa mpango huo unalenga kuinua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa. Awali mpango huo haukuweza kujadiliwa siku chache zilizopita kutokana na serikali kuuwasilisha kimakosa hali...
ZAIDI ya wafanyakazi 800 wa kampuni ya ujenzi ya chiko ya Jamuhuri ya china inayojenga barabara kuu ya Dodoma Babati eneo la mayamaya mpaka mela wamegoma wakishinikiza uongozi wa kampuni hiyo uboreshe maslahi yao kwa kuwapatia mikataba pamoja na kuongeza mishahara huku wakitaka serikali kuwafukuza wafanyakazi wa kigeni ambao wanapora ajira zinazoweza kufanywa na wazawa huku wakilipwa mamilioni ya fedha. Wakizungumza mbele ya waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa wafanyakazi hao wamesema wamechoshwa na...
Efm Radio,katika harakati zakufanikisha ahadi ya kujenga madarasa, imekabidhiwa michoro ya ramani ya madarasa ya sekondari wilaya ya Kinondoni kata ya Kimara, Makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Kituo hicho cha Utangazaji kupitia masafa ya 93.7 leo asubuhi. Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio, Francis Siza akipokea ramani ya michoro ya madarasa kutoka kwa Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bwana Rogers J. Shemwelekwa. Afisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Rogers J. Shemwelekwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Efm...
WATU zaidi ya 70 wameuawa kutokana na mashambulio ya mabomu ambayo kundi la magaidi wanaoitwa Dola la Kiislamu limedai kuyafanya karibu na sehemu takatifu ya Washia nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kituo kilichopo mjini London, kinachofuatilia haki za binadamu nchini Syria, watu hao waliuawa kutokana na miripuko miwili ya mabomu karibu na sehemu hiyo takatifu, Sayyida Zeinab. Watoto kadhaa walikuwamo miongoni mwa walioangamizwa huku Watu wengine zaidi ya 100...
NIGERIA imeomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu na nusu kutoka Benki ya Dunia ili kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake. Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani. Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani...
RAIS wa Jamhuri ya Mmuungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili. Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa tukio hilo ambapo...
SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeona picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi. Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura. Shirika hilo limeongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku...
KUNDI la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi kwa mahakama ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba. Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo. Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama...