CCM YATIMUA WANACHAMA 25 BAADA YA KUKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU
Local News

CHAMA cha Mapinduzi-CCM-mkoa wa Kigoma kimewafukuza wanachama wake 25 baada ya kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka jana. Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari, Katibu wa chama hicho mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala amesema kuwa uamuzi huo umetolewa katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama kilichofanyika machi 2 mwaka huu. Naomi amesema baada ya kufanyika kwa Uchaguzi mkuu chama kilianza kufanya tathimini na changamoto walizokutana nazo wakati wa Uchaguzi na kugundua kuwa wanachama hao ni miongoni...

Like
252
0
Friday, 04 March 2016
ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM KUANZA MACHI 9 NCHINI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi Tanzania tarehe 9 Machi mwaka huu na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.   Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake pamoja na ‎Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam. Hiyo ni ziara ya...

Like
232
0
Friday, 04 March 2016
TWIGA STARS KUSHUKA DIMBANI LEO KUKIPIGA NA MIGHTY WARRIORS
Slider

Leo wanawake wa shoka ‘Twiga Stars’, wanashuka katika dimba la Azam Complex Chamazi kukipiga na timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa Nasra Juma imejipanga vilivyo kuwakabili wazimbabwe katika mechi hiyo kwa mujibu wa kocha huyo. Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti na hamasa kwa kikosi hiko katika mchezo wake Tunawatakia kila heri katika kuleta ushindi...

Like
229
0
Friday, 04 March 2016
AZERBAIJAN: KAMISHENI YA UMOJA WA ULAYA YAIDHINISHA UJENZI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI
Global News

  KAMISHENI ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha makubaliano kati ya Umoja huo na Ugiriki juu ya ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Azerbaijan unaolenga kupunguza utegemezi wa nishati kwa Urusi. Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 878, litasafirisha mita bilioni 10 za ujazo za gesi kwa mwaka kutoka Azerbaijan hadi Italia kupitia Ugiriki, Albania na Bahari ya Adriatiki. Awamu ya kwanza ya gesi hiyo inatazamiwa kuwasili barani Ulaya mwaka 2020 ambapo Ugiriki itafaidika kwa mafao ya kodi kwa miaka...

Like
247
0
Friday, 04 March 2016
TRUMP ASHAMBULIWA NA WAGOMBEA WENZAKE KWENYE MDAHALO WA REPUBLICAN
Global News

MGOMBEA Urais Donald Trump ameshambuliwa na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono. Bwana Trump anayeongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz. Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si...

Like
196
0
Friday, 04 March 2016
TMA: MVUA ZA MASIKA ZITAKUWA ZA WASTANI
Local News

UTABIRI wa Hali ya Hewa kwa mvua za masika zinazoanza wiki hii nchini umeonesha kuwa zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi huku baadhi ya maeneo zikiwa chini ya wastani.   Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi mkuu wa malaka ya Hali ya Hewa Tanzania dokta Agnes Kijazi ambapo amesema katika maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria, Nyanda za juu, Kaskazini Mashariki pamoja na maeneo machache ya mkoa wa Tanga mvua zitanyesha hadi juu...

Like
364
0
Friday, 04 March 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA KAMATI YA UCHUMI BARIADI IKUTANE NA WAFANYABIASHARA KUPANGA USHURU
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo.   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.   Waziri mkuu Majaliwa mefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa...

Like
277
0
Friday, 04 March 2016
KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA KUJIBU VIKWAZO VYA UN
Global News

KOREA KASKAZINI imerusha makombora ya masafa mafupi, baharini kujibu vikwazo vipya ilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Jeshi la Korea Kusini limethibitisha kushuhudia shughuli hiyo na kusema kwamba havikulenga mtu yeyote. Miongoni mwa vikwazo vipya vilivyowekwa na umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo ni pamoja na kuhakikisha mizigo yote inayoingia Korea Kaskazini kutoka nje kuanza...

Like
189
0
Thursday, 03 March 2016
REPUBLICAN: TRUMP APATA UPINZANI MKALI
Global News

IKIWA tayari mwelekeo unaonesha kuwa kinyang’anyiro cha kiti cha urais wa Marekni kitakuwa ni kati ya Bi. Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican, wazee na vigogo ndani ya chama cha Republican wamesema kuwa hawapo tayari kumruhusu Trump Agombee Urais. Wakuu hao wa chama cha Republican wamesema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais wao basi kuna uwezekano mkubwa wa chama chao kusambaratika. Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South...

Like
221
0
Thursday, 03 March 2016
JAMII IMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO
Local News

WAZAZI na Walezi nchini wametakiwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na ndugu au wanafamilia dhidi ya watoto wa kike na hata wa kiume ili wachukuliwe hatua. Akizungumza na Efm Mwanasheria Msaidizi wa Jaji kutoka Chama cha Majaji Wanawake Tanzania-TAWJA-Koku Mwanemile ameeleza kuwa kufumbia macho vitendo hivyo kunachangia kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji kwa watoto. Koku amebainisha kuwa endapo wazazi, walezi na jamii wataungana pamoja kwa kufichua vitendo hivyo vinavyosababisha athari kubwa kwa...

Like
270
0
Thursday, 03 March 2016
WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM
Local News

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao za kuisaidia serikali.   Makamba ametoa wito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam.   Makamba amesema kamati hiyo ni muhimu katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe...

Like
271
0
Thursday, 03 March 2016
« Previous PageNext Page »