HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUAJIRI MAAFISA HABARI
Local News

SERIKALI imeagiza kila mkoa na kila Halmashauri nchini kuajiri Maafisa wa Habari na kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao vyote vya maamuzi pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za maafisa habari ili kuboresha mawasiliano ndani ya serikali na mawasiliano ya serikali na umma.   Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nauye, wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Kigoma, aliyoifanya kwa ajili ya kutembelea idara zilizo chini ya wizara yake ambapo...

Like
214
0
Wednesday, 06 April 2016
3 WAFUNIKWA NA KIFUSI KAWE
Local News

MTU mmoja anasadikiwa kufariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa mara baada ya kuangukiwa na kufunikwa na kifusi katika chumba kimoja   maeneo ya Kawe Ukwamani, jijini Dar es salaam . Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kawe Ukwamani SULTANI JETA amesema mnamo alfajiri ya leo kulisikika mshindo ambao ulitokana na ukuta kudondoka na kuwafunika watu wan ne wa familia moja wakiwepo watoto wawili ,mtu mzima mmoja na msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mbili ambao wote...

Like
322
0
Wednesday, 06 April 2016
RAIS WA YEMEN AWATIMUA KAZI WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA RAIS
Global News

RAIS wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi amemfukuza kazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Khaled Bahah kutokana na kile alichoeleza utendaji mbovu ndani ya serikali. Mabadiliko haya yanakuja ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa hatua ya kusimamishwa mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana katika mgogoro nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la serikali nchini humo, Rais Hadi amemteua Ahmed Obaid bin Daghr kuwa waziri mkuu huku akimteua Meja Jenerali Ali...

Like
214
0
Monday, 04 April 2016
SYRIA:VIKOSI VYADHIBITI MJI WA AL-QARYATAIN
Global News

VIKOSI vya Jeshi nchini Syria na washirika wake vimedhibiti tena mji wa Al-Qaryatain kutoka mikononi mwa Islamic State, ukiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya kundi hilo. Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya kundi la IS kuondolewa katika eneo la karibu na mji wa Palmyra. Wanamgambo wa IS waliuteka mji wa Al-Qaryatain mwezi Agosti, na kuwateka mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo Wakristo ambao wengi wao waliachiwa huru...

Like
185
0
Monday, 04 April 2016
WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUACHA TABIA YA KUWA TEGEMEZI
Local News

WANAWAKE nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wajishughulishe ili kujikwamua kiuchumi na kuepukana na ukatili wa kijinsia unaowakabili baadhi ya wanawake. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Lihundi wakati alipokuwa akizungumza na kituo hiki juu ya upingaji wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Amesema kuwa katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huo umebaini kuwa kwa asilimia kubwa ukatili wa kijinsia unawakabili wanawake ambao hawajawezeshwa...

Like
301
0
Monday, 04 April 2016
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DARESALAAM LIMEFANIKIWA KUKAMATA PIKIPIKI 519
Local News

JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata pikipiki 519 ambazo zimekuwa zikitelekezwa kutokana na makosa mbalimbali ya barbarani kutoka katika manispaa tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kamanda wa kanda maalumu ya mkoa huo kamishina Simon Sirro amesema katika kuhakikisha wanapambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo wa kutumia pikipiki jeshi hilo limefanikiwa kuzuia pikipiki nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitelekezwa na baadhi ya watuhumiwa....

Like
227
0
Monday, 04 April 2016
VIONGOZI 72 DUNIANI WAHUSIKA NA KAMPUNI YA SIRI
Global News

STAKABADHI za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa. Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi....

Like
238
0
Monday, 04 April 2016
JESHI LA NIGERIA LAMNASA KINGOZI WA KUNDI LA ANSARU
Global News

JESHI la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaidi la Al Qaeda. Taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo. Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatia kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni kwa...

Like
190
0
Monday, 04 April 2016
MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KUANZA HIVI KARIBUNI
Local News

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km. 356 kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano aliyoitoa kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi na Tabora.   Ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge mkoani Tabora, mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema ujenzi huo unatarajia kuanza rasmi hivi karibuni....

Like
413
0
Monday, 04 April 2016
CUF KUTOA MSIMAMO WAKE LEO JUU YA MZOZO WA KISIASA ZANZIBAR
Local News

CHAMA kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar CUF leo kinatarajiwa kutangaza mikakati yake na msimamo kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar. Hata hivyo msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia mufaka kati ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili. Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada wa dola 487 kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani...

Like
210
0
Monday, 04 April 2016
UGANDA: BESIGYE KUACHILIWA HURU
Global News

MKUU wa kikosi cha polisi nchini Uganda amesema kuwa atawaondoa maafisa wake nje ya nyumba ya kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye mara moja. Besigye amekuwa akihudumia kifungo cha nyumbani tangu tarehe 20 mwezi Februari,siku ambayo rais Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa taifa hilo. Hapo jana Alhamisi, Mahakama ya juu nchini Uganda ilitupilia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa rais...

Like
191
0
Friday, 01 April 2016
« Previous PageNext Page »