KATIKA kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika Disemba 9 mwaka huu, watumishi wapatao 39 wa Jeshi la Magereza nchini wanatarajiwa kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro. Washiriki hao wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani. Akizungumza na...
MFUKO wa afya ya jamii umezindua rasmi huduma ya tiba (TIKA) kwa kadi katika Manispaa ya Temeke utakao mwezesha mwananchi kupata hudua hiyo kwa gharama nafuu. Akizungumza katika ufunguzi huo, mkurugenzi wa mfuko wa afya ja jamii – CHF, bwana Eugen Mikongoti amesema kuwa mpango huo ni mpango wa hiari ulioanzishwa kwa sheria namba 1 ya mwaka 2001 ambapo chini ya mpango huo mwana jamii anaweza kuchangia kiasi cha fedha kilicho kubalika katika mamlaka ya jamii ili kumwezesha kupata matibabu...
MAMLAKA ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi na kubaini kuwa Application hiyo haina uwezo huo. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Application hiyo ya simu hivyo baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini...
MAMLAKA ya udhibiti na usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA) imeiagiza mifuko yote nchini kuzingatia kanuni na sheria zinazoitaka kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na endapo watachelewesha malipo hayo wanapaswa kulipa fidia ili kuepusha usumbufu. Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa fedha na rasilimali watu wa (SSRA) Mohamed Nyasama wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wanaotegemea kumaliza chuo cha mipango ya maendeleo vijijini (IRDP) mjini Dodoma ambapo amesema wastaafu wengi wamekuwa wakilalamikia usumbufu...
IMEELEZWA kuwa watu wenye ulemavu wanakabilwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za kijamii. Hayo yamebainishwa hii leo katika maadhimisho ya watu wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya furahisha jijini mwanza. Akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu Blandina Sembo amesema huduma za kijamii zimekuwa miongoni mwa changamoto kubwa kwa walemavu hasa wa kundi la wasiosikia kwa kukosa taarifa muhimu za...
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haina mpango wa kufunga maduka ya dawa baridi yaliyopo katika maeneo ya Hospitali za Serikali ispokuwa mpango waliokuwa nao ni kuhakikisha kuwa wanaimarisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu pamoja na kuboresha huduma muhimu ziweze kupatikana kwa ubora na haraka zaidi. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Donan Mmbando wakati wa ziara yake ya Hospitali ya Taifa ya...
KATIBU MKUU Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi. Balozi Sefue ametoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. Amesema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina...
HATIMAYE Makontena tisa yalio kamatwa jana maeneo ya mbezi tangi bovu mali ya kampuni ya HERITAGE EMPIRE COMPANY LIMITED yamefunguliwa na kukaguliwa na kukutwa na malighafi za ujenzi wa kiwanda. Makontena hayo tisa ambayo yana milikiwa na kampuni ya HERITAGE EMPIRE yameanza kukaguliwa toka jana jioni na kukamilika leo ambapo e fm imeshuhudia ukaguzi huo na kukuta malighafi mbalimbali za ujenzi kama vile vyuma vikubwa vyenye uwezo wa kujenga kiwanda cha ukubwa wa square mita za mraba elfu nne vitu...
UONGOZI wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam MUMADA waliopo Soko la Kibasila wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kurekibisha uchakavu wa miundombinu ya majitaka, mazingira pamoja na majengo ya soko hilo la Kibasila licha ya Manispaa hiyo kukusanya ushuru wa kutosha kuboresha hali ya mazingira katika soko hilo. Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Muungano wa Wafanyabiashara Masoko kanda ya Ilala Issa Malisa amesema uongozi hauko tayari kuona kampuni...
SERIKALI imesema imeanza uchunguzi wa ufisadi wa Dola milioni 6 uliohusu mkataba wa mkopo kati ya benki ya Stanbic na serikali. Jumatatu, mahakama nchini Uingereza iliamuru kulipwa kwa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania baada ya taasisi ya uchunguzi wa makosa makubwa ya ufisadi ya Uingereza kuwasilisha ushahidi kwamba kiasi hicho cha fedha kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za Serikali kwa benki ya Stanbic Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema ni uchunguzi wa benki kuu ya Tanzania...
KAMPUNI ya Uchimbaji madini ya Geita Gold Mine leo imeungana na Watanzania kuadhimisha siku ya ukimwi duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Disemba mosi kila mwaka. Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Makamu wa Rais wa kampuni hiyo Simon Shayo amesema kuwa nchi nyingi zinazoendelea zimekuwa hazipati fedha nyingi kama ilivyokuwa mwanzoni kutoka kwa Mataifa makubwa hali inayosababisha utoaji huduma kuwa mgumu. Aidha Shayo ameongeza kuwa ndoto ya mkakati wa kutoa Elimu juu ya ugonjwa huo ni kufikia mahali ambapo...