KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui. Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu. Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa...
KAMATI maalum ya muungano wa nchi zilizotia saini mkataba wa Roma wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya ICC, yenye wanachama 18 imelikubali ombi la Kenya la kukiondoa kifungu cha sheria ya 68 ya mahakama hiyo katika kesi inayomkabili Makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto. Hayo yamefikiwa baada ya hapo jana Kenya kusema iko tayari kujiondoa katika Mahakama ya ICC, iwapo haitapata hakikisho kuhusu namna kesi dhidi ya Ruto itakavyoendeshwa. ...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis leo asubuhi amezuru katika maeneo wanakaoishi watu maskini katika kitongoji cha Kangemi, Nairobi, ambapo ametoa kauli kali dhidi ya matajiri wachache wanaowatenga maskini wenye shida. Amewakosoa matajiri hao kwa kuhodhi mali ambazo zingewasaidia maskini. Akizungumza katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, Papa Francis amesema amezuru kwenye eneo linalokaliwa na watu wapatao 100,000, ili kuonyesha mshikamano kwao akiwataka wafahamu kwamba hayuko tofauti nao katika...
URUSI imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State. Rais Vladmir Putin amemwambia mwezie wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo. Rais huyo wa Ufaransa yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini...
HOFU ya umma kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa imepungua katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Kura ya maoni ya kimataifa inaonyesha kuwa hofu hiyo imepungua hasa katika nchi zilizostawi kiviwanda. Ni nchi nne pekee ambazo ni – Canada, Ufaransa , Uhispania na Uingereza ambazo kwa sasa raia wake wanaunga mkono serikali zao kuweka malengo katika mkutano wa dunia wa mazingira utakaofanyika wiki ijayo mjini Paris...
KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki dunia Papa Francis amewataka viongozi wa kikristo na Kiislamu nchini Kenya kujadiliana juu ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya Waislamu wa itikadi kali yalioikumba Kenya. Papa Francis ameyasema hayo leo nchini humo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu kama sehemu ya ziara katika nchi tatu za kiafrika. Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani amekutana na viongozi wa kidini mjini Nairobi kabla ya misa yake ya kwanza iliyohudhuriwa na...
MAHAKAMA ya Ulaya ya haki za binaadamu imekataa hoja ya mfanyakazi mmoja wa kiislamu aliyetaka kuvaa hijab kazini. Christine Ebrahimian alipoteza kazi yake katika hospitali moja ya Paris baada ya kusisitiza kutaka kuvaa hijab huku hospitali hiyo ikisema kuwa imepokea malalamiko kuhusu yeye kutoka kwa wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo. Sheria ya Ufaransa inakataza maonyesho ya uhusiano wowote wa kidini na wafanyakazi wa umma ambapo pia mahakama hiyo imesema kuwa haiwezi kutoa hukumu kuhusu sheria za wafanyikazi na kukataa rufaa...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameanza ziara yake Afrika kwa kuhimiza umoja, uwazi, kuwathamini vijana na kuyatunza mazingira. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliwasili Nairobi jana majira ya saa kumi na nusu jioni na kukaribishwa kwa shangwe na viongozi wa kisiasa na kidini uwanja wa ndege. Baada ya kuwasili, alielekea Ikulu ambako alipanda mti kisha kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kutoa hotuba yake ya kwanza, lakini awali akimkaribisha kutoa hotuba, Rais Kenyatta, alieleza umuhimu wa...
URUSI imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia kuangushwa kwa ndege yake. Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema kuwa Uturuki inawalinda Islamic State na kufafanua kuwa nchi hiyo inahofia kupoteza kipato kikubwa inachofaidika kutokana na wizi wa mafuta kutoka Syria. Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis ameondoka mjini Roma kuelekea nchini Kenya leo, ambako ataanzia safari yake barani Afrika itakayomfikisha pia nchini Uganda na katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Safari hiyo ya kwanza barani Afrika kufanywa na Papa huyo mwenye umri wa miaka 78 inatajwa kukabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama. Ratiba ya ziara ya Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani ina mambo mengi, yakiwemo kuutembelea mtaa wa mabanda nchini Kenya, madhabahu ya mashahidi wa kikristo nchini Uganda,...
JUMUIA ya kujihami ya nchi za magharibi NATO imesema inasimama pamoja na Uturuki baada ya kuitungua ndege ya kivita ya Urusi. Akizungumza baada ya mkutano wa dharura ulioitishwa na Uturuki, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki. Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande...