Slider

INDIA: 23 WAPOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA DARAJA
Global News

MAMIA ya waokoaji wakiongozwa na majeshi, wahandisi na matabibu wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha katika mji wa India wa Calcutta kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye barabara ya juu iliyoanguka wakati ikijengwa. Maafisa wanasema hadi sasa watu 23 wamekufa na mamia kujeruhuwa na wengine wakiwa bado wamefukiwa na kifusi. Inasadikiwa watu wengi wamefukiwa ambapo hadi sasa tayari watu 23 wamethibitishwa kufariki na mamia wengine kujeruhiwa ambao wanapatiwa...

Like
238
0
Friday, 01 April 2016
WATOTO WANAOTUMIWA NA WALEMAVU KUOMBA MISAADA HUSHINDWA KUHUDHURIA MASOMO
Local News

IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaotumiwa na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuomba fedha barabarani wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutumia muda mwingi kwa kazi hiyo. Akizungumza na EFM   mwanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu, Jonathan Haule amesema kuwa watoto hao wamekuwa wakitembea barabarani nyakati za masomo. Amesema kuwa ni vyema serikali ikaanzisha mifumo madhubuti itakayowawezesha watu wenye ulemavu kufanya kazi zao pasipo kutegemea...

Like
286
0
Friday, 01 April 2016
SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL
Local News

SERIKALI imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi na Arusha.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa hiyo.   Prof. Mbarawa amesema Serikali imedhamiria...

Like
267
0
Friday, 01 April 2016
MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KUTIA TIMU NDANI YA EFM REDIO
Local News

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda atia timu ndani ya EFM redio leo, ziara hiyo ni katika kuangalia utendaji kazi wa redio hiyo pamoja na kujadiliana mambo kadha wa kadha yahusianayo na jamii kwa ujumla. Mkurungenzi wa EFM redio Francis Siza katika picha ya pamoja na Mh. Paul Makonda leo alipotembelea kituo hicho. Paul Makonda akiwa studio akiongea na baadhi ya watangazaji wa kipindi cha UHONDO ambao ni Dina Marios, Swebe Santana pamoja na Sofia Amani...

Like
1133
0
Friday, 01 April 2016
TRUMP ABADILI MSIMAMO WAKE JUU YA KUTOA MIMBA
Global News

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda mfupi baada ya kusema wanawake wanaotoa mimba wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba ukiharamishwa.   Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC kauli ambayo ilimfanya kushutumiwa vikali.   Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa. Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu 1973...

Like
287
0
Thursday, 31 March 2016
WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI
Global News

WAZIRI wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.   Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua.   Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa...

Like
255
0
Thursday, 31 March 2016
SERIKALI YAKEMEA TABIA YA KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA
Local News

SERIKALI imekemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi. Kufuatia hatua hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, mheshimiwa Ummy Mwalimu amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini. Amewaonya wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa...

Like
261
0
Thursday, 31 March 2016
KIGOMA: KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA RAMI MWEZI MEI MWAKANI
Local News

MAKANDARASI wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano...

Like
1215
0
Thursday, 31 March 2016
ENGLAND: ROY HODGSON AFANYA MAZUNGUMZO KUMREJESHA JOHN TERRY
Slider

Kocha wa England, Roy Hodgson akiri kuanza kufanya mazungumzo na John Terry ili arejee kwenye kikosi kuongeza nguvu. hatua ya kocha huyu kutaka kumrejesha Terry imekuja baada ya kugundua pengo kwenye safu ya ulinzi kwnye kikosi chake kwenye michuano ya Euro 2016. Terry, 35, ambae amestaafu soka la kimataifa September 2012 anatajwa kuwa tumaini la kocha Roy...

Like
277
0
Thursday, 31 March 2016
VIETNAM: BUNGE LAPATA MWENYEKITI WA KWANZA MWANAMKE.
Local News

Bunge la Vietnam limepiga kura na kumpitisha Nguyen Thi Kim Ngan kuwa mwenyekiti wa bunge hilo kwa ushindi wa asilia 95.5% ya kura zilizopigwa. Ushindi huo wa Ngan, 61, unamfanya aingie kwenye rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kukamata nafasi hiyo ya uongozi katika taifa hilo. Kabla ya ushindi huo hapo awali Ngan alikuwa mkurugenzi wa idara ya fedha katika jimbo la nyumbani kwake la Ben...

Like
295
0
Thursday, 31 March 2016
UKRAINE: BUNGE LAHIDHINISHA HATUA YA KUJIUZULU KWA MWENDESHA MASHTAKA MKUU
Global News

BUNGE la Ukraine limeidhinisha hii leo hatua ya kujiuzulu kwa mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Viktor Shokin mtu ambaye amekuwa akionekana na nchi za magharibi zinazoiunga mkono Ukraine kama kizingiti katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Marekani imekuwa mara zote ikitaka pafanyike mageuzi kuanzia ngazi za juu katika ofisi hiyo ya mwendesha mashaka. Hata hivyo Wanaharakati wanaopinga rushwa wamekuwa wakisema kwamba ofisi ya mwendesha mashitaka huyo mkuu imekuwa na dhima muhimu katika kuyalinda maslahi ya wala rushwa na kuruhusu...

Like
281
0
Tuesday, 29 March 2016