WAZIRI WA MAMBO YA NDANI wa Ureno amejiuzulu kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa inayohusishwa na utoaji vibali vya mgawo wa makazi. MIGUEL MACEDO amesema hahusiki na kashfa hiyo lakini amejiuzulu kulinda heshima ya Taasisi za Serikali. Taarifa zimebainisha kuwa Polisi wamewakamata watu 11, akiwemo Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini humo, siku ya...
HELIKOPTA ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni Helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili . Ajali ya hivi karibuni imetokea katika viunga vya mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na Uasi wa wanamgambo wa Jihad. Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka...
RAIS BARACK OBAMA wa Marekani amesema kuna haja ya Mageuzi zaidi nchini Myanmar katika kuelekea kuipata Demokrasia. Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Yangon leo, Rais OBAMA amekosoa jinsi watu wa dini za walio wachache wanavyotendewa na pia hatua ya kumzuia kiongozi wa upinzani, AUNG SAN SUU KYI, kutogombea Urais. SUU KYI aliyeachiwa huru miaka minne iliyopita baada ya kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa takribani miongo miwili, sasa ni mjumbe katika Bunge la nchi hiyo, ingawa anashindwa kugombea...
MAREKANI na India zimesema zimepata muafaka juu ya mzozo uliohusu ruzuku ya chakula nchini India, ambayo mwaka jana ilikwamisha makubaliano ya kibiashara katika Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO. India imekataa kutia saini makubaliano hayo muhimu Julai mwaka jana, ikitaka kwanza kuhakikishiwa hazina kubwa ya chakula nchini humo. Kulinagana na makubaliano yaliyofikiwa, hazina ya chakula ya India haitakabiliwa na changamoto zozote kutokana na kanuni za WTO, hadi pale suluhisho la kudumu kuhusu suala hilo litakapokuwa...
RAIS wa Liberia ELLEN JOHNSON SIRLEAF ameondoa sheria ya hali ya hatari ambayo ilikuwa imetangazwa nchini humo katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maradhi ya Ebola, ambayo yaliizonga nchi hiyo na nyingine mbili jirani katika kanda ya Afrika Magharibi. Katika hotuba yake kwa taifa Rais SIRLEAF amesema kuondolewa kwa sheria hiyo hakumaanishi kwamba mlipuko wa ugonjwa huo umemalizika. Amebainisha kuwa Maendeleo ya kutosha yamepatikana katika vita dhidi ya maradhi hayo kuwezesha kuondolewa kwa sheria...
JESHI la Misri limesema wanamaji wake 8 hawajulikani walipo baada ya kile ilichokiita shambulizi la Kigaidi dhidi ya boti yake iliyokuwa ikifanya doria kwenye bandari za nchi hiyo katika bahari ya Mediterania. Msemaji wa jeshi hilo Brigedia Jenerali MOHAMMED SAMIR amesema kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba boti iliyofanya shambulizi hilo imeharibiwa na kwamba wavamizi 32 wamekamatwa. Mapema leo, Shirika la Habari la Misri, MENA limesema washambuliaji waliokuwa ndani ya boti 3 wameishambulia kwa bunduki boti ya doria ya Jeshi...
SHIRIKA la Madaktari wasio na Mipaka-MSF limesema kuwa wanatarajia kufanya majaribio juu ya aina tatu za dawa zinazoweza kutibu maradhi ya Ebola Mwezi Desemba katika vituo vya shirika hilo nchini Guinea na Liberia. Majaribio mengine tofauti na hayo kuhusu aina mbili ya dawa, moja kutoka kampuni ya Chimerix ya Marekani na nyingine iliyotengenezwa na kampuni ya Fujifilm ya Japan yanalenga kutathmini namna Maji ya Damu ya wagonjwa waliopona Ebola yanavyoweza kusaidia kuwatibu watu walio na maradhi hayo. Tangazo la MSF...
UJERUMANI imepanga punguzo la Kodi la Euro Bilioni 1 kuimarisha matumizi mazuri ya Nishati katika majumba na kuongeza biashara ya magari yanayotumia nishati ya umeme, katika mpango wa kusaidia uchumi huo mkubwa katika bara la Ulaya kufikia malengo yake ya utoaji wa gesi zinazochafua mazingira. Waraka wa Sera ya Nishati umeonesha kwamba licha ya kuelekea katika Nishati Mbadala , utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira nchini Ujerumani umepanda ...
ZAIDI ya Wahudumu 400 wa Afya wanaowatibu Wagonjwa wa maradhi ya ugonjwa wa Ebola katika Kliniki moja nchini Sierra Leone wamegoma. Wahudumu hao wakiwemo wauguzi na wafanyakazi wengine wanagoma kushinikiza kuwalipa Dola Miamoja kila wiki kwa kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwashughulikia wagonjwa wa hao. Kliniki hiyo iliyo mjini Bandajuma karibu na eneo la Bo, ni kliniki pekee ambayo wagonjwa wa Ebola wanatibiwa Kusini mwa Sierra Leone. Kwingineko nchini Mali, muuguzi mmoja pamoja na mgonjwa aliyetibiwa na muuguzi huyo wamefariki...
Rais wa Marekani BARACK OBAMA na Rais wa China XI JINPING leo wametangaza malengo mapya ya Mabadiliko ya Tabia nchi mwishoni mwa mazungumzo yao ya siku mbili mjini Beijing. XI amesema utoaji wa China wa Gesi zisizochafua mazingira utaongezeka ifikapo mwaka 2030, ambapo vyanzo vya nishati ambayo sio mafuta ikiwa ni asilimia 20 ya Nishati itakayotumika wakati huo. Rais wa China hakuweka lengo la viwango vya utoaji gesi ama upunguzaji, lakini ni mara ya kwanza kwa China , ambayo inategemea...
PAPA Mtakatifu FRANCIS ametaka viongozi Duniani wanaoshiriki Mkutano wa G20 mjini Brisbane kuwafikiria watu Masikini Ulimwenguni. Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa kuimarisha hali ya maisha ya watu walio masikini. Viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa wanakutana Brisbane nchini Australia mwishoni mwa juma hili kujadili maswala mbalimbali yahusuyo...