MKUU wa Wilaya ya Temeke Sofia Mjema amepiga marufuku shughuli za uchimbaji Kokoto na Mchanga zinazofanyika kigamboni pamoja na maeneo mengine ya Manispaa ya Temeke kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika kupitia shughuli hizo. Mjema amechukua maamuzi hayo baada ya kutembelea maaneo hayo akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Manispaa ya Temeke ambapo amebaini uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika kupitia shughuli hiyo huku akirejea Kauli ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Said Meck Sadick kua...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein leo ameongoza mazishi ya marehemu Bi Asha Bakari Makame aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Mazishi ya Marehemu yamefanyika huko Kianga, Wilaya ya Magharibi ‘B’, Mkoa wa Mjini Magharibi kwa heshima zote za Chama Cha Mapinduzi, ambapo viongozi mbali mbali wa vyama na serikali wamehudhuria akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi...
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mrundi Hamisi Joselyn Tambwe ameendelea kuwa kinara wa kupachika mabao katika klabu yake ya wanajangwani Yanga SC. Tambwe amefanikiwa kuirejesha timu hiyo kileleni mwa Ligi kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Timu ya Majimaji katika mchezo uliopigwa jana uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, yeye akipachika mabao 3 katika ushindi huo. Kwa ushindi huo Yanga imerudi tena kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kufikisha alama 39, sawa na Azam FC iliyopo...
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajia kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita. Rais Kenyatta atawatembelea majeruhi hao katika hospitali ya Forces Memorial iliyopo Nairobi na baadaye kujumuika na ndugu, marafiki na maafisa wakuu wa Jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa. Serikali ya Kenya bado haijatoa idadi kamili ya wanajeshi wake waliouawa baada ya kambi hiyo iliyoko El-Ade kushambuliwa ingawa Mkuu wa Majeshi nchini humo Jenerali...
WAZIRI wa Mambo ya Usalama wa Ndani nchini Somalia amesema watu 20 wamefariki baada ya hoteli mbili maarufu za ufukweni kushambuliwa mjini Mogadishu. Waziri Abdirisak Omar Mohamed ameviambia vyombo vya habari kuwa watu wengine 20 wamejeruhiwa baada ya hoteli za Lido Sea Food na Beach View kushambuliwa jana jioni. Hata hivyo tayari Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabaab limekiri kuhusika kwenye shambulio hilo ambalo limetajwa kuwa ni miongoni mwa mashambulio ya...
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mheshimiwa Ummy Mwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo lipo ndani ya Hospitali ya SekouToure, na kufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dkt John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana. Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, Waziri Ummy ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka...
RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania. Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo ya jamii kupitia nafasi zao kiutendaji. Maraisi wengine waliowahi kupata hiyo kutoka Chuo hicho ni Rais wa Awamu...
WILAYA ya Kinondoni kupitia Mkuu wa Wilaya hiyo inatarajia kuongeza shule za Sekondari ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika Wilaya hiyo. Efm Radio 93.7 katika kuunga mkono juhudi hizo za Serikali imeahidi kujenga madarasa mawili . Mkuu wa Vipindi vya 93.7 efm Dickison Ponela akipokea mchoro wa madarasa, kutoka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana, Rogers J. Shemwelekwa Katikati ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo, Scholastica Mazula na Pembeni kushoto ni Injinia wa Wilaya hiyo Bwana Brighton. Mhariri...
BOTI mbili za doria za Marekani zikiwa na wafanyakazi 10 zimekamatwa nchini Iran. Maafisa wa Marekani wamesema boti hizo zilikuwa katika mazoezi kati ya Kuwait na Bahrain kwenye eneo la Ghuba, baada ya moja wapo kupata matatizo ya kiufundi na kupoteza mwelekeo hadi katika maji ya Iran. Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani John Kery amewasiliana na mwenziye wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amemhakikishia kwamba wanamaji wa boti hiyo watarudishwa mara...
SHIRIKA linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto walioko Sudan kusini hawako shule. Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani. Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani na kwamba tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane...
WAFANYABIASHARA wa soko lisilo rasmi lililopo tegeta kwa ndevu Jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum la kufanyia biashara zao kutokana soko la nyuki lililotengwa kuwa finyu hali inayosababisha wao kuendelea kuwepo sokoni hapo. Wakizungumza na efm Jijini Dar es salaam Wafanya Biashara hao wamesema kuwa kipinndi cha nyuma eneo hilo lilikuwa lipo chini ya serikali ya mtaa ambapo kwa sasa linamilikiwa na mtu binafsi ambae ndie amewapangisha. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Soko hilo...