MANISPAA ya wilaya ya Ilala, imepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni kumi na mbili kutokana na kodi ya majengo kiasi kitakacho tumika katika kuboresha huduma za kijamii . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa uhusiano kutoka Manispaa hiyo, TABU SHAIBU amesema Manispaa ya Ilala ina vyanzo vingi vya mapato na moja ya vyanzo vikuu ni kodi ya majengo hivyo imepanga kuzunguka na kupita kila kona ya mtaa ili kuhakikisha ina wanakabiliana na wakwepa kodi ...
IMEELEZWA kuwa licha ya kupungua kwa maambukizi mapya katika baadhi ya Mikoa, kasi ya kukuwa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu imeendelea kupanda katika Mikoa ya Mwanza na Arusha ambapo katika Mkoa wa Arusha maambukizi yamepanda kutoka wagonjwa wapya 60 hadi wagonjwa wapya 111 kwa wiki na katika Mkoa wa MWanza maambukizi yamepanda kutoka wagonjwa wapya 45 hadi 66 kwa wiki. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta Ahmis Kigwangala wakati...
Kaimu meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema bado inawezekana klabu hiyo kumaliza katika nne bora Ligi ya Premia baada yao kulaza Crystal Palace 3-0 Jumapili. Hata hivyo, amekiri kwamba ni jambo ngumu. Klabu hiyo ya Stamford Bridge sasa imeenda mechi nne bila kushindwa, kwa mara ya kwanza msimu huu, na kupanda hadi nambari 14 ligini. Hata hivyo, bado wanapungukiwa na alama 13 kufika eneo la kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Ushindi wao dhidi ya Palace, walio nambari saba...
MATOKEO ya awali ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yanaonyesha Waziri Mkuu wa zamani Faustin Archange Touadera anaongoza. Wagombea 30 walishiriki kwenye uchaguzi huo ambao huenda ukaingia awamu ya pili kati ya wagombea wawili watakaoongoza tarehe 31 ya mwezi huu. Upigaji kura ulifanyika tarehe 30 Desemba mwaka 2015, huku walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakilinda vituo vya kupigia kura....
KAZI ya kuweka alama ya X , nyumba zitakazobomolewa kesho, inaendelea leo katika eneo la Jangwani baada ya mapumziko ya sikukuu za Mwisho wa Mwaka. Mwanasheria wa Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira-NEMC, Manchare Suguta, amesema wamehakikishiwa ulinzi wa kutosha Kutokana na wiki iliyopita, wananchi kufanya vurugu wakipinga nyumba zao kuwekwa alama hiyo. Suguta amesema nyumba elfu 4 zinatarajiwa kuwekwa alama ya...
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameanza ziara yake ya kikazi leo Mkoani Ruvuma. Waziri Mkuu Majaliwa aliondoka na kuwasili Mkoani humo jana, na leo atafungua tawi la Benki ya Posta Mjini Songea pamoja na kukagua Maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula-NFRA, Kanda ya Songea. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kesho anatarajiwa kutembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo na kuongea na watumishi...
WATU kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea leo ikihusisha basi kampuni ya Luwinzo linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Njombe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na ameiambia Efm kuwa bado wapo eneo la Tukio ili kuweza kutambua idadi ya watu waliopoteza maisha pamoja na...
DIWANI WA KATA YA MBAGALA KUU YUSUPH MANJI DECEMBER 31 2015 AMEITUMIA KUWASHUKURU WANANCHI NA WAPIGA KURA WA KATA YA MBAGALA KUU KWA USHINDI ALIOUPATA MANJI AMBAYE KWENYE MIPANGO YAKE YA MWAKA 2016 ILIYOANZA LEO JANUARY 01 AMESEMA ATABANDIKA NA KUSAMBAZA RATIBAYAKE YA KUTEMBELEA KILA MTAA MARA MOJA KWA MWEZI ILI KUFUATILIA UTENDAJI WA AHADI ZAKE NA KUTOA NAFASI KWA KILA MWANANCHI WA KATA YAKE AWEZE KUONGEA NAE ANA KWA ANA NA KUWAELEZA KILA JAMBO KUBWA LA MAENDELEO LITAKALOKUWA LINAJITOKEZA....
KUFUATIA Manispaa ya kinondoni kukabiliwa na tatizo la upumgufu wa shule za sekondari lililosababishwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanao faulu, Manispaa hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu imepanga kujenga shule sita ili kusaidia kupunguza sehemu ya tatizo hilo. Mkuu wa wilaya ya kinondoni PAUL MAKONDA amesema ni aibu kubwa kwa manispaa kubwa kama ya hiyo kuwa na upungufu wa shule za sekondari kutokana na manispaa hiyo kuwa na wadau wengi wenye uwezo wa kusaidia kuondoa tatizo hilo....
JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya fujo wakati wa mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa watakaokaidi amri hiyo. Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa matairi ya gari, upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zinaweza kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya....
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JOHN POMBE MAGUFULI leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea amani Tanzania utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste nchini -TFC GODFREY MALASSY amesema kuwa mkesha huo utakuwa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia Tanzania kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi oktoba mwaka huu kwa Amani na utulivu, pamoja na Dua maalum ya kumuombea Rais. Aidha ameeleza kuwa katika tamasha hilo...