Sports

AC MILAN YATWAA UBINGWA DUBAI CHALLENGE BAADA YA KUILAZA 4-2 REAL MADRID
Slider

Klabu ya soka ya AC Milan imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Dubai Challenge kwa kuitandika mabingwa wa dunia kwa upande wa klabu na barani Ulaya, Real Madrid magoli 4-2. Magoli ya AC Milan yalifungwa na wachezaji Stephen El Shaaraway aliyefunga magoli mawili, Jeremy Menez na Giampaolo Pazzini huku kwa upande wa Real Madrid yakifungwa na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema. Milan inayonolewa na kocha Phillipo Inzaghi aliyewahi kucheza...

Like
475
0
Wednesday, 31 December 2014
ALIEKUWA KOCHA WA STOKE CITY NA CRYSTAL PALACE YUPO MBIONI KUSAINI NA WEST BROMWHICH ALBION
Slider

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Stoke City na Crystal Palace yu mbioni kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu ya West Bromwhich Albion kwa kuziba nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Alan Irvine. Pulis ambaye ni mshindi wa tuzo ya ya kocha bora msimu uliopita amekubali kujiunga na klabu ya West Brom na kuitosa Newcastle baada ya mazungumzo ya kina baina yake na wamiliki wa pande zote mbili. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 amesema hakuwa...

Like
376
0
Wednesday, 31 December 2014
KOCHA WA WEST BROMWHICH ALBION AFUNGASHA VIRAGO
Slider

Klabu ya West Bromwhich Albion nimemfungashia virago kocha Alan Irvine ikiwa ni miezi saba tu toka apewe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kinachokipiga katika uwanja wa Hawthorns. Irvine raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 56 aliteuliwa kukinoa kikosi cha WBA baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pepe Mel kutimuliwa, amekuwa akipata matokeo mabovu na kuwaacha klabu hiyo katika nafasi ya 16 ndani ya msimu wa ligi kuu nchini England. West Brom inataraji kusafiri kwenda jijini London kumenyana na...

Like
362
0
Tuesday, 30 December 2014
CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA MCHEZAJI WA ULIMWENGU
Slider

Nahodha wa timu ya taifa ta Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji wa ulimwengu (Globe Soccer Award) huko nchini Dubai. Ronaldo amepata tuzo hiyo mbele ya wachezaji mbalimbali kama Messi, Neuer ambao ndio wapinzani wake wakubwa katika tuzo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani ballon d’Or inayotarajiwa kutolewa tarehe 12 januari 2015. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utoaji wa tuzo hizo, Ronaldo amesema anashukuru kwa kushinda tuzo hiyo na...

Like
518
0
Tuesday, 30 December 2014
MOUNRINHO: KUNA KAMPENI INAENDESHWA KUIANGUSHA CHELSEA LIGI KUU YA ENGLAND
Slider

Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema kuna kampeni inaendeshwa dhidi ya klabu yake ili isifanye vizuri ndani ya ligi kuu nchini England kwa kuwashawishi marefarii kutotoa maamuzi sahihi. Kocha huyo raia wan chini Ureno anayesifika kwa ubwatukaji amewashutumu makocha wenzake, watangazaji wa michezo pamoja na wachambuzi kuwa wanachangia kwa kiasi kikubwa klabu ya Chelsea kuandamwa na maamuzi ambayo siyo sahihi ndani ya uwanja. Maneno hayo ameyatoa baada ya kushuhudia mchezaji Cesc Fabregas kunyimwa penalty katika mchezo wa jana...

Like
447
0
Monday, 29 December 2014
MALI YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2015
Slider

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Mali, Cheick Omar Kone ametangaza kikosi cha awali kinachotaraji kwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwezi januari mwaka 2015 huko nchini Equatorial-Guinea. Kikosi hicho ambacho ni cha awali kabla ya kile cha mwisho kutangazwa mnamo tarehe tatu januari 2015 kimeshuhudia mshambuliaji wa klabu ya Metz, Modibo Maiga akirejea kundini baada ya kutoitwa kwa kipindi kirefu ndani ya timu hiyo. Abdou Traore na Cheick Diabate wanaokipiga katika klabu ya Bordeaux nao...

Like
380
0
Monday, 29 December 2014
GIANFRANCO ZOLA ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA CAGLIARI
Slider

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Italy, Gianfranco Zola ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Cagliari kwa kuchukua nafasi ya Zdenek Zeman. Uongozi wa Cagliari umefikia maamuzi hayo baada ya kuona matokeo mabovu chini ya kocha Zeman aliyewaacha katika nafasi ya 17 ndani ya ligi kuu nchini Italy (Serie A). Zola aliyewahi kuvinoa vikosi mbalimbali kama West Ham na watford anataraji kuanza kukinoa kikosi cha Cagliari mnamo siku ya jumapili ya tarehe 28...

Like
432
0
Thursday, 25 December 2014
DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET
Slider

Nahodha wa timu ya taifa ya Cricket, Micahel Clark amepata matumaini mapya ya kurudi uwanjani mapema kabla ya michuano ya kombe la dunia baada ya madaktari kumfanyia upasuaji wa misuli. Clark aliumia katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya India huko Adelade kwa timu ya taifa ya Australia kuibuka na ushindi wa rani 48 kwac sifuri. Australia itaanda michuano ya kombe la dunia kwa kushirikian na taifa la New Zealand kuanzia tarehe 14 mwezi wa pili mwaka 2015. Micahel...

Like
348
0
Thursday, 25 December 2014
BARCELONA MBIONI KUMUONGEZEA MKATABA NEYMAR
Slider

Uongozi wa klabu ya FC Barcelona upo mbioni kumuongeza mkataba wa miaka miwili nahodha wa timu ya taifa ya Brazil na mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar utakaomalizika mwaka 2018. Mkataba wa sasa wa Neymar unataraji kuisha mwaka 2018 ila kiwango kizuri alichokionyesha Mbrazil huyo kimewashawishi viongozi hao kutaka kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia asijiunge na klabu nyengine. Neymar amefanikiwa kuunda mahusiano mazuri na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji hatari duniani Lionel Messi pamoja na Luis Suarez....

Like
457
0
Tuesday, 23 December 2014
CHELSEA YAILAZA 2-0 STOKE CITY
Slider

Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Stoke City na kujihakikishia nafasi ya kwanza kuelekea katika msimu wa sikukuu ya Christmas. Magoli ya Chelsea yamefungwa na beki na nahodha wa klabu hiyo John Terry huku kiungo wa Kihispania Cesc Fabregas akifunga goli la pili la mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Brittania. Chelsea imefikisha alama 42 ikiwa ni 5 dhidi ya klabu ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili huku historia ikionyesha...

Like
441
0
Tuesday, 23 December 2014
BARCLAYS PRIMIER LEAGUE: CHELSEA KUMENYANA NA STOKE CITY LEO
Slider

Vinara wa Ligi kuu nchini England, klabu ya Chelsea leo wanashuka tena dimbani kumenyana na klabu ya Stoke City katika uwanja wa Brittania majira ya saa tano kamili usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki. Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 39 sawa na klabu ya Manchester City iliyopata ushindi mnono wiki iliyopita dhidi ya Crystal Palace. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemuomba refarii wa mchezo huo wa leo, Swarbrick awe makini katika maamuzi...

Like
402
0
Monday, 22 December 2014